Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]


           *TWO MEN ~ ONE MESSAGE.*
Tokeo la picha la WHY WE WANT YOU TO BE RICH by DONALD J. TRUMP & ROBERT T.KIYOSAKI.
                 
                     SEHEMU YA TATU

            *SURA YA KUMI NA SABA*

ULIPOKUWA JESHINI ULIFUNZA NINI AMBACHO KITAKUSAIDIA AU KINAKUSAIDIA KATIKA MAISHA YAKO?
👉🏻Mwandishi wetu KIYOSAKI anasema yeye kwamba alipenda kwenda jeshini kwa sababu tatu muhimu ambazo ni;

📌Alipokuwa na miaka kumi Mwalimu wake wa darasa la tano aliwa waambia kuhusu historia ya wapelelezi wakubwa mfano Columbus,Cortez,Magellan na Da Gama,hii ilimuhamasisha ROBERT kuendelea na safari za majini na kupeleleza kuhusu dunia /ulimwengu mzima.

👉🏻Kuna siku moja kiongozi wake wa shule alimuuliza kwamba anapenda nini akija kuwa mkubwa KIYOSAKI akajibu anapenda kusafiri katika safari za majini,kunywa bia na kupata wanawake wazuri.Ndipo yule mwanamke akampeleka katika mafunzo ya kijeshi.

📌Anasema sababu nyingine iliyompelekea yeye kwenda jeshini ni kwa sababu wazazi wake walikuwa hawana fedha za kumpeleka chuo au kumsomesha chuo.

📌Anasema hii ya tatu na inawezekana ni muhimu sana ilikuwa ni Nidhamu,anasema nidhamu ilikuwa ni muhimu kwa sababu anasema hata kama angeenda chuo cha Hawaii asingemaliza chuo.

👉🏻Anasema katika mafunzo yoyote Nidhamu ni kitu muhimu sana,anasema kutokana na mafunzo ya jeshi alikuwa amepata mafunzo muhimu ya kupewa oda na kutoa oda na anasema kifupi alijifunza masuala ya uongozi.

👉🏻Utofauti wa shule za kijeshi na shule za biashara, ukweli ni kwamba katika shule ya kibiashara kuna mambo kama;

📌Bidhaa/zao

📌Masuala ya kisheria

📌Mfumo wa biashara.

📌Mawasiliano.

📌Mzunguko wa fedha.

👉🏻Ila katika shule ya jeshi kuna mambo makuu matatu ambayo ni;

📌Umoja

📌Maono makubwa/Mipango

📌Uongozi

👉🏻Mwandishi wetu anasema kwamba alitumia miaka minne akiwa katika shule jeshini na akafanyakazi karibia miaka sita katika huduma za kijeshi anasema hii ilimu andaa yeye kupambana na uhalisi wa ulimwengu wa ujasiliamali na masuala ya uwekezaji. Na anasema ilikuwa ni elimu muhimu kwa sababu alijifunza mambo kama.

📌Nidhamu

📌Mtazamo

📌Kuwa na mipango mikubwa kuliko anavojiona anaweza kutekeleza.

📌Kufuata maagizo na kutoa maagizo.

📌Kudhibiti uogo na hasira.

📌Kumsoma adui na kumheshimu adui.

📌Kujenga uaminifu na wanajeshi wenzake.

📌Kujia andaa vyema kabla ya kuingia uwanja wa vita.

👉🏻DONALD anasema yeye alipokuwa jeshini alijifunza kuongoza katika umoja,pia alijifunza kwamba kuweka visingizio vya kushindwa jambo fulani havitakiwi katika maisha yake.

👉🏻DONALD anasema pia faida nyingine aliyoipata kutoka kwenye shule ya jeshi anasema hapendi kulalamika kuhusu mambo fulani yakiwa yanaenda sivyo.

👉🏻  Je ulichojifunza katika shule yako ya jeshi/ jeshini kitakusaidia katika maisha yako na je ni kivipi?
_______________________________________________

👉🏻Kama hukwenda jeshini je ulipokuwa katika skauti na vikundi vingine vya mambo ya kijeshi je umejifunza umuhimu wa nidhamu na uongozi?
_______________________________________________

👉🏻Je ni wapi katika maisha yako utafanikiwa zaidi ukiwa na Nidhamu kubwa ( katika masuala ya fedha na masuala ya muda) na ujuzi wa uongozi?
_________________________________________________

                      YOU MUST BECOME A RICH
                      Ahsante,
     Usikose kesho sura ya kumi na nane ya kitabu.
                     Phone.0742364499.
      Email.mwanyikajackson428@gmail.com.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]