Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]

Tokeo la picha la WHY WE WANT YOU TO BE RICH by DONALD J. TRUMP & ROBERT T.KIYOSAKI.


           *TWO MEN ~ ONE MESSAGE.*

                  SEHEMU YA TATU

        *SURA YA KUMI NA NANE*

JE ULIJIFUNZA AU UNAJIFUNZA NINI KUTOKANA NA MICHEZO ULIYOCHEZA AU UNAYOCHEZA?
👉🏻Mwandishi wetu ROBERT anasema yeye amewahi kucheza michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu ambayo ilikuwa ni mojawapo ya mchezo aliyowahi kucheza katika ukuwaji wake na anasema alijifunza mambo tofauti tofauti ambayo yaliathiri maisha yake!

👉🏻Katika michezo aliyowahi kucheza alijifunza kama ifuatavyo;

📌Anasema katika ligi ndogo alijifunza kucheza kwa jitihada hata kama tayari katika timu yao hawa nafasi ya kushinda, alijifunza hata kama utapoteza nafasi ya kushinda mara kadha utajikuta siku moja unashinda hii ni kwa sababu utaendelea kujichunguza na kufanya mabadiliko chanya na kuwa washindi badae!

📌Katika Golf alijifunza kudhibiti hisia,mawazo na mwili wake,anasema Golf ni rahisi kwa nadharia ila ni ngumu sana kucheza kwa hiyo sheria iliyopo kwenye Golf huwa anaitumia kwenye biashara kwa sababu hufanana.

📌Katika mchezo wa surfing anasema alijifunza yeye kama mwekezaji kujua kipindi gani cha kuingia kwenye soko na kutoka katika soko.

📌Katika mchezo wa kuendesha Boti alijifunza kuwa na umoja.

📌Katika mchezo wa mpira wa miguu alijifunza wajibu wakila mcheza na kazi zake akiwa uwanjani.

📌Katika mchezo wa  aina kama basketi,alijifunza hata kama umechoka kiasi gani unatakiwa kukimbia ili kusaidia wachezaji wengine na timu yako kiujumla.

📌Katika mchezo ambao unahusisha mapigano mfano kareti na judo hapa alijifunza kwamba nguvu ya mwili huwa inazunguka katika mwili mzima.

👉🏻Pia katika mchezo wa mpira alijifunza kwamba kuwa na hamasa pekee haitoshi,ni muhimu kujiona mshindi katika maisha hata kabla huja shinda tayari *, halafu pia kuna tofauti kubwa kati ya kutarajia kufanya kitu fulani na kuanza kufanya hicho kitu.*

👉🏻Siko zote ukitaka kubali matokeo katika maisha yako hakikisha unabadili mawazo/ fikra zako hapo ndipo utabadili matendo yako na badae kubadili hayo matokea Katika maisha yako.

👉🏻Katika sheria ya ushindaji ni kwamba kama ilivyo katika ushindani wa michezo ndivyo inavyokuwa katika maisha ya mwanadamu yani unapotaka kuwa mshindi unahitaji kujiandaa vyema.
Na kama ushindi siyo muhimu, watu wasinge weka alama,utake usitake tunaishi katika Dunia ambayo ina weka alama.

👉🏻 *Joe Montana aliwahi kusema Kurudia rudia jambo fulani ni Mfalme* . Pia alisema  mtu yeyote ambaye anahitaji kufanikiwa sehemu fulani aliyo changua anahitaji kufanya jambo hilo na kujiandaa ipasavyo,ina maana kama uta taka kuelewa kuhusu kitu fulani ni muhimu kufanya hicho kitu kwa umakini na kwa mtazamo mkubwa . Unapofanya kitu hii inakusaidia kujua udhaifu na nguvu uliyonayo,Unapoamua kufanya kitu siyo sawa na kutarajia kufanya hicho kitu pia ni muhimu kuendelea kufanya hicho kitu bila kuacha.

👉🏻Donald anasema alijifunza kuwa na nguvu ya mwili na kutumia mbinu muhimu katika mambo yake,mfano utakuta mtu anafanya kazi kwa jitihada kubwa lakini kila siku yuko pale pale hii ni kwa sababu mtu anakosa mbinu za kumfanya apate matokeo zaid katika mambo anayofanya.

👉🏻Donald anasema katika michezo mitatu aliyo wahi kucheza alijifunza mambo makubwa matatu ambayo ni;

📌Kuwa na usahihi.

📌Silika

📌Mwendokasi .

👉🏻 *Je wewe huwa unajifunza nini unapokuwa uko kwenye michezo au ukiwa unaangalia mchezo fulani???*
________________________________________________


                      YOU MUST BECOME A RICH
                      Ahsante,
     Usikose kesho sura ya kumi na tisa ya kitabu.
                     Phone.0742364499.
      Email.mwanyikajackson428@gmail.com.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]