Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]

Picha inayohusiana

Natumaini ni mzima wa afya nakuletea hatua 101 ambazo ukizifuata unaweza kufanikiwa katika maisha yako katika kila nyanja ya maisha yako iwe kiafya,kielimu,kibiashara na hata katika masuala ya imani.Hatua hizi zinatolewa kila mwisho wa wiki yani ijumaa na jumapili ili kukuandaa wiki inayofuatia baada ya kufanya vibaya wiki ambayo imekwenda kuisha au hata kukuhamasisha pale ulipo fikia  na kujitathimi unatakiwa ufanye nini ili kuwa katika mafanikio ya hali ya juu sana.

Hatua hizi zinatolewa kila mwisho wa wiki mara mbili kama nilivyoeleza hapo juu na hatua hizi zitaishia siku ya Jumapili 22 september 2019 kama unaweza kupanga malengo maalum panga kabisa halafu siku ya mwisho tutathimini tumefanya nini panga kisiri siyo kila mtu ajue,andika kwenye noti halafu tuta tathamini.
Kwa wewe ambae umekosa mtaji anza wiki hii au kesho hakikisha kila siku unaweka 1000/= baada ya siku hizi 364 utaona unakuwa na kiasi gani!?

 NB;Zimebaki siku 357 ili kufikia malengo yetu na kumaliza hatua hizi karibu sana anza nami leo!

Panga malengo yako maalum twende kwa pamoja na mimi nitakuwa nakupa hatua mbili kila wiki kwa mfuatano hatua moja mpaka hatua ya mwisho 2019.

 HATUA YA TATU

     003 . KUWA NA NDOTO KUBWA MAISHANI
👉🏻Unapotaka kupanga malengo au ukiwa na lengo la kufanya jambo fulani lazima na pia ni  muhimu kuwa na ndoto kubwa ya jambo hilo unalotaka kufanya.

👉🏻Ili ufanye mambo makubwa katika maisha yako lazima uwe na ndoto kubwa katika mambo hayo hata kama ukiwa na ndoto kubwa kiasi kwamba unajiogopa ni muhimu kwa sababu hata kama hutazifikia lakini utajihamasisha kufikia malengo makubwa.

👉🏻Mfano kama wewe ni mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari ni vema kuwa na ndoto yakuwa TO lakini hata kama hutatimiza ndoto hizo inawezekana ukawa kwenye kumi bora ya taifa.

👉🏻Leo katika makala yangu ya kwenye kitabu cha  WE WANT YOU TO BE RICH  waandishi wamesisitiza sana katika sura ya kumi na mbili kwamba unapotaka kufanya lolote ni vema kufikiri kwa mapana zaidi, kwa maana nyingine pia ni muhimu kuwa na ndoto kubwa.

📒Kama huku soma makala yangu ya kitabu cha WE WANT YOU TO BE RICH soma jifunze unavyotakiwa kufikiri kwa mapana zaidi hata kama uko katika hali ngumu ya kimaisha.


 NB;Kama bado hujapanga malengo angalau moja tu,Tafadhari panga  andika lengo lako katika notibuku halafu tengeneza mchakato utakaofanya kila siku wa kuhakikisha lengo hilo unatimiza na mimi nitakuwa na kukumbusha kuendelea kuwa katika mchakato maalum kila mwisho wa wiki!


👉🏻Step 003 is DARE TO DREAM.


                     101 STEPS TO SUCCESS
              Achive your goals,
       Phone,0742364499.
Email.mwanyikajackson428@gmail.com.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]