Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]


kimondo cha Mbozi

Kupiga picha kwenye kimondo cha Mbozi ni tukio la kipekee kwenye kivutio cha utalii kilichopo wilayani Mbozi, mkoa wa Songwe, Nyanda za Juu Kusini nchini Tanzania. "Wengi huwa wanafurahia kupiga picha kwa sababu ni kitu cha kipekee na tunaamini kuwa mtu akishapiga picha anakuwa balozi wa kimondo hiki kwa wengine," anasimulia Beatus Bonabana, Mhifadhi, kivutio cha Kimondo Mbozi, anaongeza akisema. 'Katika miaka ya nyuma, wenyeji wa eneo hilo walikuwa wanakitumia sehemu hiyo kwa ajili ya maombi ya kupata kitu, walifanya matambiko, ni jambo linaloendelea kufanyika mpaka leo." Kimondo cha Mbozi kinakadiriwa kuwa na uzito wa tani 12 na ni cha nane kwa ukubwa duniani.


Ni cha pili Afrika baada ya kimondo cha Hoba chenye tani 60. Kimondo cha Hoba kilichopo nchini Namibia ndicho kikubwa zaidi Afrika na duniani. Haijulikani ni lini hasa kimondo hiki cha Mbozi kilianguka, ila mtu wa kwanza kukiona katika miaka ya 1930 alijulikana kwa jina la Halele Simbaya, ambaye alikuwa mhunzi. Halele alipogundua kimondo hiki alitoa taarifa kijijini kwao, ndipo wenyeji wakaanza kuabudia katika shimo ambalo huwa linahifadhi maji ambayo wenyeji hunawa kupata baraka na wakalita jambo hilo kuwa ni kusafisha nyota. "Wenyeji walikuwa wanakatakata kimondo hicho, wakaita kipande cha nyota na hata sasa wenyeji wanakiita kimondo cha nyota. Watu walikata ili kusafisha nyota, ulinzi ulipowekwa ilisaidia," Bonabana alieleza. Zamani kimondo hiki kilikuwa kinang'aa lakini sasa kimekuwa na rangi nyeusi baada ya kuathiriwa na hali ya hewa. Kimondo hiki hakifanani na chuma aina nyingine kutokana na ugumu wake na ukikipiga ni kama kuna uwazi ndani yake, unasikika mlio wa sauti ambao ni tofauti.


No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]