Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]

Tokeo la picha la MILLION DOLLAR HABITS by BRIAN TRACY

                                SURA YA KWANZA

       TABIA YAKO INATOKEA WAPI
👉Jambo lolote unalofanya kwa kurudia huweza kuwa tabia,na tabia hii endapo utairuhusu kuendelea kuwepo hufanywa kuwa tabia ya kudumu na huwa inaambata na kukufunga wewe kama mnyororo wa chuma,
👉🏻Umezaliwa ukiwa na uwezo mkubwa sana ambao huwezi kutumia wote kwenye maisha yako hapa duniani.
👉🏻Ukweli ni kwamba mambo ambayo umeyafanya ni baadhi ya mambo madogo sana ukifananisha na uwezo ulionao ndani yako,hii ni kutokana na historia alioandika mwanasaikolojia ABRAHAM MASLOW,
👉🏻Lakini changamoto iliyopo ni kwamba unapokuja duniani na uwezo wako mkubwa wa mafanikio hakuna mwongozo na maelekezo kivipi utatekeleza uwezo wako ulionao,kwa hiyo matokeo yake watu wengi hawafanyi na hawatekelezi na kuonyesha uwezo wao.
 UFUNGUO WA MAFANIKIO
Mwandishi anasema alikuwa anajiuliza swali kwa nini baadhi ya watu wanamafanikio makubwa kuliko wengine!? Na hususani kwa nini wafanyabiashara baadhi wanamafanikio makubwa kuliko wengine!?.
👉🏻Mwandishi baada ya maswali anasema akaanza kuwa na tabia ambazo zingemletea mafanikio katika maisha yake yajayo na yambele zaidi.Na akaanza kuuliza wale wafanya biashara wakubwa wanafanya mambo gani ya tofauti na yeye na ndipo akaanza kufuata tabia zao na alipo fuata aliyo ambiwa akaanza kufanya vizuri kwenye kampuni yake.
👉🏻Biblia "inasema ombeni nanyi mtapewa" (mathayo7:7),mwandishi ametumia maneno haya akimaanisha kwamba unapo uliza swali au jambo lolote la mafanikio kwa watu wenye mafanikio makubwa watakusaidia na utapata njia sahihi ya kufanya vizuri katika hilo jambo ulilokuwa na uhitaji nalo na pia ni muhimu njia utakazopewa kuzifanyia kazi.
👉🏻 Sheria ya kusababisha na athari hii ni sheria ya msingi ya falsafa ya magharibi na ya mawazo ya kisasa,sheria hii inasema kwamba katika kila kisababishi kuna athari zake,maana yake kila jambo hutokea kwa sababu fulani, na kutokana na sheria hii hatakama hujui sababu basi kila jambo linatokea kwa sababu fulani
 Ukifanya jambo au mambo ambayo watu wenye mafanikio makubwa wanafanya na wewe pia utafanikiwa na kama hutofanya basi hutofanikiwa kamwe .
👉🏻Unaweza kujifunza chochote,Mwandishi ansema katika tafiti zake kwamba mwanadamu anaweza kujifunza jambo lolote na akaweza kabisa kufanya bila pingamizi yeyote.
👉🏻 Sheria ya udhibiti ,Ni muhimu kudhibiti maisha yako, kuna sheria moja inaitwa sheria ya dhibiti inasema kwamba unajisikia furaha kwenye maisha yako kwa sababu unaweza kudhibiti maisha yako na huwezi kuwa na furaha kama huwezi kudhiti maisha yako.
Falsafa ya kisasa inasema kwamba locus of controry theory (sehemu ya nadharia ya udhibiti),
Wanasaikolojia wametofautisha kati ya sehemu ya udhibiti ya nje na ndani,wakimaanisha, kuna sehemu mbili udhibiti wa ndani ni wa mtu mwenyewe bila kutegeme hali ya jamii na watu wanao kuzunguka na udhibiti wa nje ni ule kutoka na mazingira na watu wanaokuzunguka.
👉🏻 Sheria ya kuamini hii ni sheria ya msingi ambayo ipo kwenye dini,saikolojia na falsafa,sheria hii inasema kwamba chochote unchoamini huwa kinakuja kuwa uhalisia.
 Agano jipya ktk biblia inasema kwamba kulingana na imani yako,ndivyo itavyofanyika kwako na Agano la kale vile mtu anavyoamini ndivyo hivyo
Lakini uhalisia ni kwamba hatuamini mambo tunayoyaona lakini tunayaona tuliyokwisha kuamini.
👂🏼Hutakiwa kuwa na imani ambayo itakuzuia kufikiria mambo makubwa,watu wengi wanaimani ambayo inawazuia wao kufanya mambo fulani,mambo unayoyaamni badae huwa ni uhalisia wako.
👉🏻Unapotaka kuwa na tabia za mafanikio ni lazma uhakikishe unazuia na kuondoa mawazo mgando ambayo yanakuzuia wewe kuamni mambo makubwa,
👉🏻Ukweli ni kwamba hamna kitu kigumu kubadili kama imani ya mtu kuhusu kitu fulani,lakini pamoja na hilo kila kitu duniani unaweza kujifunza kwa sababu imani huja kwa kujifunza kumbe inaweza kuondolewa na kuacha kabisa kwa kuwa na tabia za mafanikio.
👉🏻 Sheria ya uvutano ,sheria hii inasema tunaishi duniani kama sumaku kwamba tunauwezo wa kuwavuta watu,mawazo na vitu mbalimbali kutoka na fikra zetu.sheria ya uvutano ni muhimu sana hasa katika mafanikio ya kila mmoja,kwa sababu kama utafikiria chanya utapata mambo chanya na kama utafikiria mambo hasi basi utayavutia mambo hasi kwako wewe!
Hakikisha mawazo na fikra zako na ubongo wako unaujaza fikra chanya hii itakusaidia kuwa na mafanikio, furaha na amani ktk maisha yako.
👉🏻 Sheria ya mlinganyo,sheria hii inasema kwamba jinsi uavyoonekana kwa nje ndivyo ndani yako ulivyo,kwa hiyo jinsi unavyo wafikiria watu na mahusiano yako basi huwa yanaakisiwa kwako vilevile

👉🏻UNAPOWEZA KUZITUMIA SHERIA HIZI VIZURI KWA PAMOJA HAPO NDIPO UTAKUWA UMETUMIA SHERIA ZA ULIMWENGU
                                          SURA YA PILI

      MPANGO MKUU WA MAFANIKIO
👉🏻Siri ya mafanikio ni kujua hatima yako na baada ya kujua hatima yako ndipo uanze kufanya mambo kulingana na kujua ile hatima yako.
👉🏻Swali la kujiuliza kuhusu mafanikio ni vipi utangundua unayoyafikiria muda mwingi katika maisha ya yako na pia kwa nini watu wengine wanakuwa na mawazo chanya na yenye kujenga na wanakuwa na mipango ya mafanikio wakati wengine hawako hivyo,
👉🏻Mwandishi anasema watu wengi waliofanikiwa walipo ulizwa swali kwamba vitu gani wanafikiria muda mwingi katika maisha yao ? Anasema kifupi ni kwamba majibu yalikuwa wao wanafikiria kuhusu mambo wenye uhitaji nayo na watapataje hayo wanayohitaji katika huo muda mwingi.Lakini watu wasio na mafanikio wao wanafikiria vitu ambavyo hawavipendi muda mwingi na wanachukia matatizo yao na magumu wanayopitia.
👉🏻Kutoka na ile sheria ya uvutano tuliopitia jana kwenye sura ya kwanza sheria hii huwa ipo katika (neutral) kwa hiyo kutokana na kwamba hawa ambao hawana mafanikio kuchukia matatizo basi wanajikuta matatizo yana ongezeka kwao na wale wenye mafanikio basi wnavutia mafanikio kwao.
👉🏻Dhana binafsi au kujiona mwenyewe ulivyo ndani yako, kama utakuwa umeweka dhana chanya katika eneo fulani au kwa kitu fulani unachotaka kufanya badae na ukatumia dhana hiyo ndani yako na ukajiona tayari umeshakuwa ulivyokuwa unatamani kuwa hivyo utaanza kufanya mambo kulingana na mahitaji yako.
Mfano,kuwa na dhana binafsi unamvuto kiasi gani kwa jamii ndivyo utakapo jiweka ili uwe na mvuto na hii itakusaidia wewe kuwa kama unavyohitaji  kuwa na mvuto.
👉🏻Kulidhika mapema na mazoea mabaya,siku  zote mtu anaweza kuwa na uwezo mkubwa na siyo wakawaida ila mazoea na kulidhika mapema kunaweza fanya mtu kuwa wakawaida kama watu wengine, mtu anayepanga mambo yake kwa ukubwa zaidi atafanyakazi na kutoa muda mwingi kulifanya jambo mpaka ahakikishe analimaliza,ila mtu akipanga jambo dogo na akamaliza mapema hawezi kujishughulisha tena,mfano mtu akipanga kupata milioni 5 kwa mwaka atafanya kazi mpaka afikishe ile fedha na mtu akipanga afikishe milioni 20 kwa mwaka lazima atafikisha na akifikisha basi hawezi kufanya juhudi kuongeza tena zaidi ya hiko kiasi,kwa hiyo sasa mazoea inabakikuwa kikwazo kikubwa cha mafanikio na kufanya mambo makubwa,ili kutoka kwenye mfumo wa mazoea unatakiwa kubadili dhana binafsi na kubadili tabia kufanya mambo makubwa zaidi.
👉🏻Jitengenezee mwenyewe mipango mikubwa ya mafanikio, kuna usemi usemao kwamba kwenye udaktari utambuzi mzuri kwa mgonjwa ni nusu ya kumponya mgonjwa
👉🏻Dhana binafsi imegawanyika katika sehemu tatu na tuone jinsi hizi sehemu zinavyoshirikiana kila moja na zinafanyaje kazi ilikufanya na kukuwezesha unachokitaka.
  1.Ubora wako binafsi, hapa ni ile picha ambayo wewe binafsi unajiona,unaweza ukawa unajiona ni mtu mwenye mafanikio makubwa mno hata kama upo katika mazingira magumu kiasi gani,
Ubora wako binafsi mara nyingi unajengwa na ndoto,malengo na nk kuhusu maono yajayo,ikijumuishwa na ubora na mambo mema ambayo wewe unayakubali na kwa watu wanaokuzunguka.Na watu waliofanikiwa huwa wanajua ubora wao wenyewe binafsi.
Pamoja na kwamba utakuwa na picha ya ubora ubinafsi ndani yako unahitaji haya;-
💜unahitaji kuwa na watu kama mwongozo wako ambao wao ni chanya kwako na wakusaidie kukutengeneza vizuri.
💜Unahitaji kutengeneza vizuri utu wako,unatakiwa kujua thamani yako na unatakiwa kuhakikisha unatengeneza utu wako ili ufanikiwe zaidi na zaidi,thamani yako itakuja pale utakapokuwa unafikiria kile unachokihitaji wakati ujao na kwa sababu ya kanuni ya uvutano lazima kile unacho kihitaji kitakuja kwako.
  2.Unajionaje wewe binafsi, kuna mwandishi mmoja wa kitabu kinaitwa PSYCHO-CYBERNETICS kimeandikwa na Dr.MAXWELL MALTZ,tunajifunza kwamba mara nyingi mtu alivyo kwa ndani huoneshwa na yale aliyotenda kwa nje!,kama utajiona kwa ndani ni chanya,maarufu na mwenye mafanikio ndani yako, hivyo ndivyo utakavyoweza kufanya mambo kwa nje,( kwenye ulimwengu wa kawaida)
Dhana yako binafsi huwa inatwa kioo cha ndani yako na kioo hiki huwa kinaonesha uhalisia wako kabla hujaamua kufanya jambo fulani katika maisha yako,
Mfano ,kama unajiona mwenyewe ni mtu wakujiamini na unamafanikio kabla hujaonana na mtu mpya,kazi mpya au kufanya mkutano fulani basi ndivyo itakavyokuwa kwenye ulimwengu wa kawaida, kwa hiyo mojawapo ya tabia ambazo ni muhimu kuzijenga ni hii yakujiona tayari uko vizuri kabla hujafanya jambo fulani.
  3.kujiheshimu binafsi,unapojiheshimu na kujikubali binafsi hii inakupa nguvu kwa utu wako na kuongeza ufanisi wako wakufanya mambo ambayo umeyapanga.Wasaikolojia wamekubaliana na ukweli kwamba kujikubali binafsi ni sehemu kubwa ya utu wa mtu na mara nyinyi unaweza ukagundua na kutumia kujua kwamba utakuwa na mafanikio au kushindwa kuwa na mafanikio.
👉🏻Ukweli kwamba ni kwamba unapojikubali mwenyewe binafsi ni muhimu zaidi kwa sababu inasaidia kupanga maisha yako kwa ufanisi
👉🏻Kuna kanuni moja inaitwa KILA KITU KINAHESABIKA ni kwamba kila kitu kinachokutokea na kila kitu kinacho kuzunguka kina athari katika kujikubali kwako kwa namna fulani.kwa hiyo kila kitu kinachotokea kwako huwa kinaweza kushusha au kuongeza kujikubali kwako.
👉🏻Linganisha tabia yako na ubora wako,mojawapo ya mambo muhimu ni kwamba umbali kati ya picha yako binafsi, vile unavyojiona mwenyewe kwa sasa na uhalisia wako/bora wako halisi,ndivyo itakuwa hivyo kwenye maisha yako ya mbele.
👉🏻Pale unapojiona uwezo wako wa sasa wakufanya mambo na tabia inaendana na yule mtu mwenye mafanikio ambaye unaweza kufanana ile uwezo wako wa kujikubali unaongezeka sana.
👉🏻Unapojipenda mwenyewe ni rahisi kujikubali mwenyewe na ndio unapokuwa na furaha na unakuwa na mipango mizuri ya mafanikio.
👉🏻Moja wapo ya tabia nzuri za kuzijenga ni kujiongelesha mwenyewe mambo chanya na mambo ambayo unapenda ya tokee kwako hii inasaidia kujenga utu wako na moja wapo ya neno la muhimu nikusema najikubali sana
👉🏻Msingi wa utu *,je dhana yako binafsi inatokea wapi!?*inaanzaje? Na inakuwaje!?
Ukweli ni kwamba kila mtoto anapozaliwa huwa hana hii dhana yake binafsi ingawa dhana hizi hujengwa kulingana na ukoaji kutoka utotoni hadi uzeeni,
Mwanadamu amefundishwa kuamni mambo fulani hii ni kutokana na jamii inayo mzunguka inavyo amini kuhusu mambo fulani
👉🏻Ukweli ni kwamba kila mtoto huwa anazaliwa na karama fulani za kipekee sana, baadhi ya wanasaikolojia wanasema kwamba 60% ya baadhi ya tabia watu huzaliwa nazo mfano ushujaa,kupenda muziki na uwezo wa kukimbia nk,na ndio maana utakuta mtoto mmoja katika familia fulani yeye pekee ndie mwenye uwezo huo ukilinganisha na wengine ingawa wazazi wao ni walewale.
👉🏻Uhalisia bora wa kuzaliwa nao upo katika sehemu mbili;
    1.Tulizaliwa bila uoga,ila jamii ndio inatufundisha uoga mfano wazazi ndio wenye kuathiri sana watoto wao kwa kuwapa uogo kuhusu mambo mfano,mzazi atamwogopesha mwanae akimwona nyoka hii inapelekea hata mtoto kuanza kuogopa nyoka ktk maisha yake.
  Kuna uogo wa kutoweza kufanya jambo fulani,uoga wa kukataliwa na nk
   2.Tulizaliwa tukiwa na uasilia,mwanadamu anapozaliwa huwa tunauasilia wa kulia,kupiga kelele,na kujielezea wenyewe lakini wazazi huwa wanazui watoto kulia wakati fulani,kwa kuwa hakikishia kwamba wasipolia ndio wata wapenda na wakilia hawawapendi watoto,hivyo mtoto hukua kwa kuwa hakikishia wanzake au kutowakiki wenzake mpaka utu uzima hii inabadilisha uasilia wa mtoto na mwanadamu kiujumla!
👉🏻MBINU ZA KUONDOKANA NA UOGA,
Ukweli ni kwamba uoga ulionao na jinsi unavyojikubali huwa vinaenda tofauti,kwa maana nyingine ni kwamba wewe unavyojikubali hivyo ndivyo unapokuwa huogopi kushindwa na kukataliwa!
👉🏻Timiza uwezo wako kamili kwa kusoma sheria hizi nne!
1. Sheria ya tabia, ,inasema ikiwa utafanya jambo lolote kwa kurudia rudia basi hufunyika tabia kwako.
2 .Sheria ya hisia Inasema kila jambo unalolifanya ni kutokana na hisia ya jambo fulani,hilo jambo huwa ni chanya au ni hasi!
3. Sheria ya mkusanyiko inasema Chochote kama utakitilia mkazo na kukikuza na kuongeze kwenye maisha yako basi huwa kinakuwa zaidi.kwa maana nyingine ni kwamba kitu chochote uunapofikiria kwa muda mrefu basi hukua
4. sheria ya ufanyaji kazi ya akili isiyofikika inasema akili yako isiyofikika huwa inapokea mawazo, mipango na malengo ambayo yametengenezwa na akili ya kawaida na badae akili isiyo fikika huwa inabadili na kukuhamasisha malengo na mipango kuwa katika uhalisia kwenye maisha yako.
👉🏻Ukweli ni kwamba tabia za mafanikio ni muhimu na pia tabia nzuri ya mafanikio ni pale unapohakikisha akili yako inalenga zaidi kwa yale unayo yahitaji na  malengo yako kiujumla
👉🏻Your potential is ulimited and your will be assure of these by taking complete control of your self concept!
                    DEVELOP YOUR GOOD HABITS
        
                             SURA YA TATU

            KUWA MTU WA THAMANI
👉🏻Malengo hupelekea madhumuni;madhumuni hupelekea kuchukua hatua; Na hatua ulizochukua ukirudia rudia hatua hizi hufanywa kuwa tabia; Na tabia ambazo unazo ndizo huwa sifa zako ;Na sifa zako ndizo zitakazotambulisha kuwa hatima yako itakuwa ni ipi hapo badae.(Tryon Edwards)
👉🏻Mambo yote ambayo unafanya na jinsi ulivyo yanatokana na mawazo uliyonayo,hisia na tabia ulizonazo.Asilimia tisini na tano ya mawazo yako na vile vitu unavyofikiria,unavyojisikia kufanya mambo katika maisha yako huwa yanajulikana kutoka na tabia zako.
👉🏻Ukweli ni kwamba ili uje kuwa mtu wa thamani na kuwa na mafanikio makubwa katika maisha yako ni lazima ujenge tabia za kimafanikio ambazo zitakufanya wewe kupata kitu chochote unachohitaji katika maisha yako!
👉🏻Unaweza kuwa na tabia yoyote kwa sababu tabia hujengwa kwa kurudia rudia mara kwa mara kile kitu au tabia unayoihitaji,mfano unaweza ukajenga tabia ya kuamka kila siku asubuhi saa kumi na moja na nusu, kwa mara ya kwanza ni lazima uweke alam lakini baada ya muda unaweza kuamka bila hata kuweka alam hii inatokana na kurudia rudia jambo fulani badae linakuwa ni tabia yako.
👉🏻Jinsi ya kutengeneza tabia na muda ambao mpaka tabia mpya inajengeka kwako,mwandishi anasema tabia inaweza kujengwa kwa muda wowote kuanzia sekunde moja ile ambayo wewe umeamua kuwa na tabia fulani mpya mpaka miaka mingi.lakini uharaka wa tabia hutegemea zaidi kiwango cha hisia za mhusika ambazo huambatana na maamuzi ya kuanza na matendo ambayo yatapelekea tabia mpya kwa mhusika.Mfano,Daktari akimwambia mgonjwa kwamba ni lazima apunguze uzito wake asipofanya hivyo atakufa kutokana na afya yake,kwa hiyo kumbe kupunguza uzito siyo kazi ya siku moja ni ya muda mrefu zaidi,pia mgonjwa atajitahidi kufanya hivyo kwa sababu hisia zake zitakuwa anaogopa kufa ndipo atakuwa na tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara bila kuzembea,Wanasaikolojia wanaita significant emotional experience (SEE)
👉🏻UKWELI NI KWAMBA TABIA ZILIZONYINGI HUCHUKUA MUDA WA SIKU 21 HADI KUJENGEKA KUWA TABIA RASMI IJAPOKUWA TABIA NYINGINE HUCHUKUA MUDA MREFU KUJENGEKA !
👉🏻 Hatua saba ambazo zitakusaidia kujenga tabia mpya: Mwandishi amejaribu kufafanua hatua ambazo zinaweza kukusaidia kujenga tabia mpya za mafanikio ambazo ni;-

 Kwanza,Chukua maumuzi Amua kwa uhakika kwamba utakwenda kufanya jambo fulani kwa asilimia mia moja, mfano ukisema kwamba utabadili tabia fulani amua kwa uhakika na ufanye kabisa!

 Pili,Usiruhusu maneno ambayo yanapunguza hamasa mfano neno "isipokuwa" pale unazongumza kujenga tabia mpya kifupi ni kwamba usiwe na sababu ambazo zitapelekea wewe kutofanya asilimia mia moja ya lilejambo ulilosema utalifanya maana kama hutafanya kwa jinsi ulivyo panga unajidanganya mwenyewe.

 Tatu,Waambie wengine , mfano marafiki zako,mwenza wako na wale watu wajirani na nk,kwamba utakwenda kufanya jambo fulani katika maisha yako,faida ya kuwaambia wengine ni kwamba lazima utahakikisha kwamba unafanya kwa sababu utakuwa na hofu ya kwamba wale uliowaambia wanakuangalia je nikweli utafanya!?

 *Nne,Ujenge tabia ua taswira ya kujiona tayari unaile tabia uliokuwa umepanga kujenga na tayari unafanya na umekuwa vile ulivyotakiwa kuwa ,Unavyoendelea kijenga taswira kwenye akili yako kwamba umekuwa na ile tabia uliyokuwa unataka kuwa hii itakupelekea kuanza kufanya mambo au jambo mapema kulingana na ile taswira uliyo nayo.

 Tano,Tengeneza maneno ya uthibitisho ambayo utakuwa unayazungumza kwa kurudia rudia,uzapojisemesha maneno , mfano  kama ulitaka kuwa na tabia ya kuamka asubuhi saa kumi na mbili ukirudia rudia maneno haya mara kwa mara kila muda au baada ya muda fulani uliojiwekea itakusaidia kukujengea tabia hiyo mapema sana,

 Sita,Ni muhimu kuhakikisha unaendelea kuwa na tabia hiyo bila kubadilika mpaka tabia mpya ijengeke na iwe sehemu ya maisha yako na mpaka pale itakapokuwa ni rahisi kufanya kwako kama maisha mengine ya kawaida kwako.

 Saba,Hii ni muhimu sana pale unapoona tayari umeweza kubalidili tabia na imekuwa sehemu ya maisha yako basi jipe zawadi na pongezi kwa juhudi ulizozifanya mpaka kuwa na tabia fulani ya kimafanikio.

👉🏻 Jinsi ya kuondokana/kuishinda tabia ya ughairishaji wa mambo katika maisha yako, pia Mwandishi amezungumzia ni njia zipi na hatua zipi uzichukue ili kuhakikisha unaondokana na tabia ya kughairisha mambo,njia hizo ni hizi hapa;-

 Kwanza,Chukua hatua mapema zaidi kwa lile jambo uliloamua kufanya katika muda fulani

 Pili,Siku zote usiruhusu maneno ambayo yatakufanya uchelewe kufanya jambo maneno mfano neno isipokuwa.

 Tatu,Waambie watu wajirani kama marafiki kwamba utakwenda kuacha tabia yako ya kughairisha mambo.

 Nne,Jenga taswira kwamba jambo ulilotaka kufanya tayari umeshafanya na umelimaliza kulifanya .

 Tano,Jenga tabia ya kurudia rudia kulisema lile unalo taka kufanya, mfano "Nina kwenda kuanza na kuamka kila siku asubuhi na mapema"

 Sita,Jenga nidhamu mwenyewe kwamba utaendelea kufanya jambo hilo mpaka liwe tabia kwako na katika maisha yako.

 Saba,Jipongeze kwa kuishinda tabia ya ughairishaji wa mambo! Ni muhimu kujipongeza kama kweli umehakikisha umetekeleza ulilokusudia kufanya katika muda maalum.
👉🏻Baada kuwa tabia fulani mpya jifanyie tabia hiyo kuwa ni rahisi kwa maisha yako,kuwa mvumilivu na mwenye subira wewe mwenyewe, jizungumzishe maneno ya mambo ambayo utakwenda kufanya hii inasaidia kuwa na uhakika wa kufanya mambo.
👉🏻Tabia yoyote ya maisha yako ukisha kuwa nayo au kama ulikuwa nayo huwa haifi maana yake huwa haipotei,lakini unapoacha kuifanya na upojenga nidhamu ya tabia mpya ,zile tabia za zamani huwa zinakuwa dhaifu na zinaondolewa kwenye akili yako isiyofikika,kwa hiyo tabia mpya zinabadili zile tabia za zamani ila tabia za zamani huwa hazitoki kabisa zinaweza kurudia endapo utashindwa kuendeleza tabia mpya!
👉🏻 Being and Becoming maneno haya kwa kiswahili huwa na maana moja ila mwandishi ametofautisha kama ifuatavyo,
 Being ~human being
ukweli ni kwamba wewe ni mtu pekee duniani, hakuna kama wewe duniani kote,na kitu kinacho kutofautisha ni akili yako,na uwezo wako wakufikiri,kuamua na kutenda mambo!
Ndio maana unaitwa human being ~being

💜Jumla ya mawazo yako na uzoefu wako wa zamani upo ndani ya mambo unayofanya sasa au siku ya leo.
Kumbe basi kutokana na hiyo sababu we are human becoming maana yake ni kwamba tutakuwa watu fulani kutokana na tabia na mawazo ambayo tunayo leo hapo tutakuwa tunavyo taka!
 Humani becomingness

👉🏻We are not just  a human being, we are a human becomingness
      

               DEVELOP YOUR GOOD HABITS,

                          SURA YA NNE,

             TABIA UNAZOTAKIWA KUWA NAZO ILI UFANIKIWE
👉🏻Moja wapo ya tabia muhimu katika maisha yako ni tabia ya kuwa na nidhamu binafsi, Bwana Elbert Hubbard,alisema kwamba
 Nidhamu binafsi maana yake ni ule uwezo wa mtu kuhakikisha kwamba kile alichokusudia kufanya anafanya,kwa wakati mwafaka hata kama hajapendezwa kufanya au amependezwa kufanya,
👉🏻Tabia ya nidhamu binafsi huwa inaambatana na ile sheria ya udhibiti ambayo tuliona katika sura zilizopita,tujikumbushe sheria ya udhibiti ilikuwa inasema kwamba "Unajisikia furaha ndani yako kwa sababu wewe ndiye unayedhibiti maisha yako binafsi", Kumbe nidhamu binafsi ni ufunguo wa mwongozo wa maisha yako na itakusaidia kudhibiti maisha yako kwa kadri unavyotaka yawe!
👉🏻Chanzo cha nguvu ya mtu binafsi,ukweli kwamba kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya nidhamu binafsi ya mtu na mtu kujiheshimu binafsi,maana yake ni kwamba jinsi unavyo ongeza nidhamu binafsi kwenye maisha yako ndivyo unavyo jiheshimu na kujikubali binafsi na ndivyo unavyo jifikiria chanya na kuwa na ujasili wa kufanya mambo katika maisha yako.
👉🏻 Tabia ya kujenga matumaini,siku zote wenye matumaini makubwa katika maisha yao huwa wanafuraha,wanaafya njema na wanakuwa ni watu wenye athari chanya katika jamii ukilinganisha na wale wenye tabia ya kukata tamaa,Kutoka na kitabu kiitwacho LEARNED OPTIMISM alicho andika Dr,Martin Seligman,anasema kwamba watu au mtu yeyote anaweza kujifunza kufikiri mambo kwa matumaini kama watu wenye matumaini walivyo,hii ni kutokana na kwamba mtu anaweza kuwa vile anavyotaka kulingana na jinsi anavyojifikiria muda mwingi.
      💚Unapokuwa na matumaini makubwa katika maisha yako unatengeneza afya na unaongeza kinga ya mwili hii ni kutokana na utafiti wa kidaktari uliofanyika ktk eneo la PSYCHONEUROIMMUNOLOGY na utafiti huu ulitoa hitimisho hilo kwamba jinsi unavyofikiri ndivyo unaweza kupunguza au kuongeza kinga ya mwili wako.
       💚Unapokuwa na matumaini makubwa katika maisha yako, una kuwa na furaha muda wote kwa sababu utakuwa unazungumza na kufanya mambo unayotaka muda wote wa maisha yako.
      💚Watu wenye matumaini huwa wanajipanga kufanya makubwa katika maisha yao,kwa sababu wanamatumaini kwamba watafanya na wanauhakika ukilinganisha na watu wa kawaida, na kuwa na uhakika wakufanya makubwa na malengo kuwa na malengo makubwa ni tabia nzuri ya mafanikio.
       💚Watu wenye matumaini huwa wana maono katika maisha yao,siku zote wenye matumaini huwa wanafikiria mambo na maisha yao ya badae yatakuwaje na wanaanza kuyaishi ijapo wapo katika maisha yao ya kawaida ya wakati huo,moja wapo ya tabia muhimu kuwa nazo nikuwa na maono ya mbali ya maisha yako.
       💚Watu wenye matumaini makubwa huwa wanafikiria sana kuhusu malengo yao walio jipangia na watu wenye mafanikio wao pia wana tabia hizi,ukiwa unafikiri kuhusu malengo yako ni lazima utakuwa una malengo fulani ambayo yanapimika na jinsi au mipango jinsi ya kuyafikia malengo hayo.
Mwaka 2003,katika utafiti uliofanyika nchini MAREKANI kuhusu watu kupanga malengo ya maisha ifikapo kipindi cha mwaka mpya ulipata hitimisho kwamba,
      (a).4% ya watu waliopanga malengo yao bila kuandika ndio waliofanikiwa,
      (b).46% ya watu waliofanikiwa ni wale waliopanga malengo yao na wakaandika malengo yao.
Ukiangalia hapo ukweli ni kwamba kutokana na huo utafiti kulikuwa na tofauti ya 1100% ya mafanikio baina ya pande mbili,
👉🏻Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na malengo na pia kuwa na malengo tuu haitoshi lazima kuyaandika malengo hayo kwenye kumbukumbu maalum na kuyarudia rudia kuyasoma ili yawendani ya akili yako.

NJIA SABA ZITAKAZO KUSAIDIA KUTENGENEZA MALENGO,
Mwandishi anasema kwamba ni bora kuwa na lengo fulani kuliko kuto kuwa na lengo,hizo ndio njia za kukusaidia kutengeneza malengo yako,
  Kwanza,Fanya maamuzi kitu gani unataka au unakitaka katika maisha yako au eneo ulilopo na uandike vizuri na kuhakikishe hiko kitu kinapimika,
 Pili,Hakikisha unaandika siku maalum ya kutimiza lengo lako ,lengo kubwa gawanja katika malengo madogo madogo na kuweke tarehe maalum za kutimiza malengo hayo.
 Tatu,Hakikisha unaandika kila kitu ambacho kitakusidia kuweza kufanikisha kutimiza malengo yako,
  Nne.Weka malengo yako katika mpango kazi, na mpango kazi huwa unawekwa kalingana na vitu viwili ambavyo ni kipaumbele na mlolongo
👂🏼Unapoweka mambo kwa kulingana na vipaumbele maana yake unafanya vitu vya muhimu zaidi ili kutimiza lengo lako,hapa kuna sheria ya 80/20,maana yake 20% ya unayoyafanya yatapelekea 80% ya matokeo. Na usipoweka mambo katika vipaumbele utaendelea kufanya mambo madogo madogo yasiyokuwa na matokeo makubwa,
 👂🏼Unapoweka malengo katika mlolongo hii inakusaidia kufanya mambo ambayo unatakiwa kufanya kabla ya mambo mengine.
 Tano,Onyesha vikwazo na changamoto ambazo zinaweza kusababisha kushindwa kutimiza lengo lako utajiuliza swali kwa nini nimeshindwa kutimiza hili lengo!?,itakusidia kujua ni jinsi gani na njia gani utapambana na changamoto utakazo kutana nazo.
 Sita ,Baada ya kufanya mambo yote hapo juu fanya lile jambo lilopo kwenye akili yako kwa wakati mapema, fanya kitu ambacho mapema kinaweza kuanza kusaidia kufikia lengo lako.
 Saba,Hakikisha unafanya jambo kila siku ambalo litakusaidia kufikia malengo yako na tengeneza tabia ya kuwa na mipango midogo ambayo itakusaidia kufikia lengo kubwa kila siku,Panga siku yako asubuhi na kabla hujaenda kulala usiku,kabla ya siku ya mbele.
👉🏻 Ni muhimu kuwa na tabia ya kufanya kitu muhimu ambacho kitapelekea kutimiza malengo yako.Na hakikisha unapanga malengo kila siku kwenye maisha yako.
💚Watu wenye matumaini huwa wanajenga tabia ya kufanya mambo yao kwa usahihi na uhakika zaidi.
👉Ni muhimu kujua ujuzi wako vizuri watu waliofanikiwa imeonekana wanaujuzi wao zaidi ya ambao hawajafanikiwa wakiwa katika shughulizao na katika masuala ya kifedha.
👉🏻Jifunze zaidi kila siku kwenye maisha yako hii itakusaidia kukua kwa fikra,hii ni tabia ambayo ni muhimu kwa kukuza ujuzi wako, utu wako na kipato chako!
👉🏻 Mambo matatu yanaweza kukusaidia kuwa na fikra pevu na ujuzi wa haraka mahali ulipo ;
 👂🏼kwanza,Hakikisha kila siku kabla ya kwenda kwenye mihangaiko ya maisha maana yake baada ya kuamka  unasoma wastani wa dakika 30 hadi 60 katika eneo lako la kazi au kitu unacho kipenda.
👂🏼Pili,Hakikisha unajenga tabia na ratiba ya kuhudhuria semina mbali mbali katika eneo lako, mfano mjasiliamali awe na ratiba ya kuhudhuria semina za kijasiliamali.
👂🏼Tatu,Jenga tabia ya kusikiliza kanda za sauti,hii ni muhimu kwa watu wavivu wa kusoma vitabu na wale wenye kazi kama madereva ambao hawana muda wa kutulia na kusoma vitabu.
👉🏻Kila mwanadamu ndio anaweza kutengeneza hatima yake na maisha yake,hakikisha unajijengea tabia njema na malengo ili kufanikiwa katika maisha yako.
👉🏻Vile unavojiona uko ndivyo itakavyokuwa katika maisha yako badili mtazamo wako jenga tabia ya kujiona mshindi pale ulipo tengeneza malengo fuata na tengeneza mpango kazi maalum ili ufanikiwe na kutimiza malengo.
👉🏻Hakikisha unalisha akili yako mara kwa mara lisha manufaa,vitu chanya hii itakusaidia kuona fursa katika maisha yako na kuongeza kinga ya mwili.
👉🏻Tengeneza urafiki na watu wakubwa,jihusishe na watu wenye mafanikio watu unaowakubali ambao wanaweza kujenga katika kile unachokihitaji kwa maisha yako,Dr.DAVID McMCLELLAND aliwahi kusema ukitaka kujua mafanikio au kushindwa kwa mtu fuata au watafute marafiki zake au kundi la watu anaojihusisha nao.
👉🏻Chukua hatua na fanya mambo ambayo yatakupeleka kwenye malengo yako,Hakikisha umejipanga kufanya mambo, maana yake kama ni fursa imejitokeza chukua hatua mapema kutekeleza hilo jambo na hapa ndipo tunapata utofauti wa washindi na washindwaji hii ni kutokana na jinsi ya kuanza kufanya mambo katika maisha.

👉🏻You can do it,once you determine your ideal future,set and determined your goals and plans,developed a strategy for achieving excellence in your field!



                                        SURA YA TANO,

            TABIA ZITAKAZO KUFANYA KUWA MILIONEA ,
👉🏻Mwanzo wa tabia huwa mfano wa nyuzi ndogo ambazo kwa macho huwa hazionekani,lakini kwa kurudia rudia tabia hizi mara kwa mara ndipo tabia hizi zinajengeka na huwa kama zile nyuzi ndogo unapoziongezea nyuzi nyingine badae huwa kama kamba nene na yenye uwezo mkubwa bila kukatika!,hii ni kutoka na usemi wa Bwana  (Orison Swett Marden.)
👉🏻Watu waliowengi duniani kiujumla huwa wanamalengo ya kupata fedha kiasi kingi kwa kadiri ya matakwa yao wawapo katika kazi zao,ili kuwa na uhuru wa kifedha na wengine huwa wana malengo ya kuwa milionea,Kwa bahati mbaya kuwa milionea siyo rahisi kwa dunia tulionayo!
👉🏻Jifunze kufikiria kama milionea,kwenye sura zilizopita tulijifunza mara nyingi mtu anavyofikiri atakuwa ndivyo hivyo huwa ni kweli kwamba atakuwa hivyo,kwa hiyo kama unahitaji kuwa milionea jifunze kuwa na fikra kama za watu ambao ni milionea.
👉🏻Kitu kikubwa ambacho watu milionea wanafanya ni kufikiria kwa muda mrefu kuhusu kuwa huru kifedha.
👉🏻Jenga tabia ya kutunza fedha kiasi fulani kutoka kwenye mshahara wako,kwa bahati mbaya zaidi watu wengi wamejengwa na tabia ya kuwa na matumizi kuliko kutunza fedha katika maisha yako.
👉🏻Sehemu ya kuanzia ili uwe huru kifedha kwenye maisha yako ni lazima uhakikishe kwamba unatimiza wajibu wako kuhusu masuala ya kiuchumi katika maisha yako.Kibaya zaidi watu wengi hawajui kuhusu hili wanafikiria kuwa na hela ni bahati nzuri za watu,wanajikuta wakiingia kwenye michezo ambayo siyo sahihi na wanahofu kubwa kuhusu masuala ya fedha.
👉🏻Ukweli ni kwamba fedha ya msingi ni ile unayoitengeneza kwa muda mrefu,Watu matajiri duniani huwa wanahakikisha kwamba kila mwaka uchumi wao wa kifedha unapanda 8%--10%,kifupi ni kwamba huwa wavumilivu na huwa wanasubira kwenye masuala ya kifedha,na pia huwa wana nidhamu ya kutunza fedha na kukusanya kwa muda wa miaka mingi!
👉🏻Jitengenezee akili yako kuwa kama ya watu milionea,kuwa milionea siyo vigumu kama tunavyodhania lakini pia siyo muhimu kuwa milionea, jambo la muhimu ili uje kuwa milionea ni jinsi unavyo kusanya fedha yako ili uwe milionea kwa mara ya kwanza!,
👉🏻Ili uwe tajiri katika maisha yako unatakiwa kuwa na tabia, fikra na akili kama za matajiri na pia ni muhimu kuwa na malengo yako maalum ya kuhusu masuala ya fedha,
Mwandishi anasema mshauri wake wa kifedha alimwambia kwamba kuwa milionea kwa mara ya kwanza ni vigumu sana ukilinganisha na ukiwa milionea kwa mara ya pili,maana yake ni kwamba ukiwa milionea mara ya kwanza basi hatakama utapoteza fedha yako yote kuwa milionea tena ni rahisi sana kwa sababu itakuwa ni tabia yako kuwa hivyo!.
👉🏻 Tabia za watu milionea mwandishi ameainisha tabia za watu tajiri kama ifuatavyo ;-
 💚Watu matajiri duniani huwa wako makini na matumizi ya fedha zao,ukweli ni kwamba watu wenye mafanikio ya kifedha duniani huwa wako makini kwenye matumizi ya fedha,wanatumia fedha zao kiuchumi zaidi,mfano watu matajiri huwa hawa nunui gari mpya badala yake huwa wana nunua gari zilizotumika,kwa sababu ukweli ni kwamba gari mpya baada ya mwaka mmoja huwa zinashuka 20% ya thamani yake,pia gari zilizo nyingi hupungua 30%--50% ya thamani zake baada ya miaka miwili.
💚Watu matajiri huwa wanatabia ya kuhifadhi na kutunza fedha zao,Bwana W.Clement Stone alisema kwamba,''Kama hutaweza kutunza fedha zako vyema basi hutaweza kuja kuwa mtu mwenye fedha kwenye maisha yako''
 George Classon ,katika kitabu chake cha Richest Man In Babylon amezungumza kwamba mojawapo ya ufunguo mkubwa wa mafanikio ni pale mtu anapojilipa mwenyewe na alisisitiza kwamba jitahidi utunze angalau 10% ya mshahara wako kabla ya matumizi yako ya kawaida, katika maisha yako yote,na hii 10% ndio ile unayojilipa wewe mwenyewe!
👉🏻Kwa kawaida tabia yeyote hujengwa na kujifunza na badae huwa ni tabia ya mtu,watu wengi wapo kwenye madeni leo kwa sababu hawana tabia ya kujilipa wenyewe!kwa ni muhimu kujenga tabia hizi za kifedha za kujilipa mwenyewe kabla ya matumizi mengine!
👉🏻Unapojenga tabia ya kuhifadhi na kutunza fedha ni vizuri kwa sababu utaongeza fursa ambazo zitakuongezea kupata kipato kikubwa na kuwa na fedha zaidi.
👉🏻Jifunze kupenda kutunza fedha kuliko kutumia fedha watu wengi duniani wamefunzwa kutumia fedha zaidi kuliko kutunza kutoka na sura ya kwanza ya kitabu tulisema tabia ni Conditioned response to stimuli maaana yake ni kwamba kadiri unapoendelea kufanya kitu fulani mara kwa mara huwa kinajengeka na kuwa tabia ya kudumu kwenye maisha yako.
👉🏻Badili fikra zako,watu wengi wanakuwa na furaha wanapotumia fedha katika maisha yao kwa ajili ya starehe na mambo mengine,na pia huwa wanajisikia vibaya wanapotakiwa kujibana ili kutunza fedha zao na wajekutumia fedha zao kwa mambo ya msingi ya maisha yao ya badae,lakini wewe unatakiwa na kuwa na mtazamo tofauti jisikie vibaya unapotumia fedha zaidi kuliko unapotunza fedha zaidi.
💚Watu matajiri wanatabia ya kujisikia vibaya pale wanapotumia fedha kuliko wanapohifadhi na kuwekeza fedha zao kwa ajili ya maisha yao ya badae!na kifupi ni kwamba watu matajiri duniani huwa wanakuza utajiri wao taratibu!
Ukweli ni kwamba watu matajiri duniani huwa wanatumia muda wao zaidi kufikiria kuhusu fedha kuliko watu wa wakawaida,matajiri wanatumia mara 10 zaidi ya watu wakawaida kila mwezi.
👉🏻Ukweli ni kwamba kwa kawaida mtu kipato chake kinavyopanda basi na matumizi yake huongezeka na matumizi huongezeka ili kulingana na kipato chake hii ni kutokana na sheria ya parkinson's !
💚Watu matajiri huwa wanatabia ya kupata ushauri mzuri wa kifedha kabla hawajafanya jambo lolote la kifedha, kifupi ni kwamba ni muhimu kuwa na mshauri mzuri wa kifedha!pia ni muhimu kuwa na tabia ya kufanya uchunguzi kabla ya kufanya uwekezaji wa aina yeyote,tumia muda mrefu kufanya uchunguzi ili kufanya uwekezaji
 👉🏻Ukweli ni kwamba utajiri siyo sababu ya kuwa na maisha mazuri,ila ukweli  wa maisha ni kwamba lengo la maisha kwa mwanadamu ni kuwa na furaha.
👉🏻The ultimate end or purpose of all human life is the achievement of personal happiness,
        

                                DEVELOP YOUR GOOD HABIT

                                                SURA YA SITA,

             TABIA ZITAKAZO KUFANYA ULIPWE ZAIDI NA UKUE ZAIDI MAHALI ULIPO,
👉🏻Mtu yeyote ambaye anahitaji kufanya biashara vizuri na kuwa mfanyabiashara mkubwa lazima ujenge na uzingatie nguvu ya tabia na lazima uhakikishe kwamba unazingatia umuhimu wa tabia za mafanikio.
👉🏻Kuna kazi na vitu vingi vya kufanya ambavyo vita kufanya ulipwe zaidi na uwe huru kifedha lakini ni muhimu kujenga tabia ya kupenda unachokifanya kuliko kufanya kazi au kitu chochote ili mradi tu kipo au ulihitaji kufanya kwa muda fulani!
👉🏻Jenga tabia ya jitathimini kitu gani unakipenda kufanya kwenye maisha yako na una karama au kipaji gani katika maisha yako hii itakujenga wewe kupenda kufanya mambo unayoyapenda kwenye maisha yako!
👉🏻Kila mtu amezaliwa na kitu ambacho ni cha kipekee kwenye maisha yake, kama ilivyo kwamba kuna aina nyingi za akili,na wewe unaweza ukawa na karama au akili mbalimbali,utakuwa na furaha na maisha mazuri pale unapofanya kitu unacho kipenda kwenye maisha yako!

 KAZI BORA KATIKA MAISHA YAKO
👉🏻Dr.Victor Frankl,mwanzilishi wa tiba za alama ,alisema kwamba kuna aina nne za kazi ambazo mtu anaweza kufanya kwenye maisha yake,ambazo ni;-

 💚 Kwanza,Kazi ambayo ni ngumu kujifunza na ni ngumu kufanya ,hizi ni kazi mfano kazi za uhasibu na uhifadhi wa masuala ya fedha ambazo hazi husiani na ujuzi wa mtu aliozaliwa nao.,Itakuwa ni kazi ngumu hata kama utafanya kwa miaka mingi zaidi maishani!,watu wengi wamejikuta wakifanya kazi ambazo hazihusiani na vipaji au karama zao,mfano kuna mtu anafanya kazi ya udaktari lakini siyo karama yake mtu huyu atafanya kazi hii kwa muda mrefu bila kuwa na furaha au kutoipenda kabisa,kwa hiyo usifanye kitu usicho kipenda!

 💚 Pili,Kazi ambayo ni ngumu kujifunza ila ni rahisi kufanya ,hii ni kazi kama ujuzi wa kuandika kwenye compyuta au kuendesha ndege au gari ni kazi ambazo unahitaji kuwa makini na kutumia muda mwingi kusoma na kujifunza ila ukisha jifunza ni rahisi kufanya kwenye maisha yako.Kazi hii huchangia kiasi kidogo cha kujigundua karama yako

 💚 Tatu,Kazi ambayo ni rahisi kujifunza lakini ni ngumu kuifanya ,Hizi ni zile kazi ambazo wengi wetu wanafanya mfano kazi za kibeba mizigo ,kulima kwa mikono na nk,kazi hizi huwa ni ngumu hata ufanye muda mrefu kiasi gani!,Kazi hizi huwa hazina karama yoyoye!
💚Nne,Kazi ambazo ni rahisi kujifunza na nirahisi kufanya, Hapa ndio watu wengi wanapendakuwa kwenye kazi ambazo ni rahisi kujifunza na kufanya,kwa bahati mbaya kazi hizi zinahitaji uwe na kipaji na ufanye jambo lile unalo lipenda kwenye maisha yako!, Mara nyingi huwa ni kazi za watu wanaopenda vitu vyao na kuzaliwa na karama hiyo!
👉🏻Jitengenezee utaratibu kwa kufanya unayoyapenda hayo yatakufanya ufurahie unapoyafanya pia yatakufanya ulipwe zaidi kuliko kufanya usiyo yapenda mfano,unapofanya kazi unayoipenda maaana yake utafanya kwa moyo na utaifurahia zaidi na itakufanya ulipwe zaidi,
👉🏻Ukweli ni kwamba unapojenga tabia ya kujitathimini kipi au kazi gani unapenda kufanya kwenye maisha yako hii inaongeza ubora wa maisha yako, kwa hiyo ni muhimu kutumia muda mrefu kutathimini,kujitambua na kufikiria kipi unapenda kufanya kwenye maisha yako,ambacho itakuwa ni kazi na itakufanya ulipwe zaidi katika maisha yako.
👉🏻Unapokutana na fursa za kazi usiwe na haraka yakupata kazi tumia muda mwingi kutambua ni kazi ipi utaifanya kwa ufasaha na utaipenda kwa moyo na itakufanya ulipwe zaidi.
👉🏻Siku zote unapohitaji kufanya kazi yeyote uwe umeajiriwa au umejiajiri usiwe unahitaji zaidi kuhusu ulinzi wa hiyo kazi bali angalia zaidi fursa !
👉🏻Sahau yaliyopite tazama zaidi kuhusu maisha yajayo,Unaweza ukatumia muda mwingi kusoma halafu ukakosa kazi,Unaweza kuwekeza muda au fedha kwenye kitu fulani halafu ukapata hasara(sunk cost),usiogope ila tafuta fursa ambazo zitakufanya ujenge maisha yako yajayo!
👉🏻Ukisha tambua kipi unapenda kufanya kwenye maisha yako basi hakikisha unafanya kwa ufanisi mkubwa na hakikisha unapata taarifa stahiki ili kufanya jambo hilo kwa ufanisi mkubwa maana tuko dunia ya mabadiliko ambayo yanakwenda kwa haraka,
👉🏻Tumia muda mrefu kuchagua kazi unayo ipenda ili ufanikiwe kwenye maisha yako, kuliko kuingia kwenye kazi yeyote ili mradi tuu unafanya utashindwa kufanikiwa.

 TABIA MBILI ZITAKAZO KUFANYA UKUE ZAIDI ULIPO
👉🏻Mwandishi anasema kwamba hizi ndizo tabia ambazo zitakufanya ukue kwa haraka hapo ulipo na ndio siri kubwa za mafanikio kuliko nyingine zote,Tabia hizi zitakusaidia wewe muajiriwa,maneja,mjasiliamali na hata mfanyabiashara mkubwa,
Ni rahisi kujifunza lakini zinanguvu kubwa ya kukuuzua mahali ulipo tabia hizo ni;

 💜 Kwanza,Tabia ya kuanza kitu au kazi mapema,kufanya kwa juhudi na kuchelewa kuondoka kama ni kazini ,hamna kingine zaidi ya siri kwa kawaida kazi huanza saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni,Lakini wewe unatakiwa uamke mapema na uanze kazi saa moja na nusu hadi saa mbili au moja usiku,
👉🏻Ukweli nikwamba unapowahi kufanya kazi nankufanya kwa juhudi na ukachelewa kuahirisha kazi hiyo basi unaongeza uzalishaji kwa 50%--100%,na watu au marafiki wakigundua unajituma watakuwa tayari kukusaidia wewe na kukufanya ukue zaidi kwenye kazi yako!

 💜 Pili,Tabia ya kuomba na kutimiza wajibu wako, mfano kwa muajiriwa hakikisha unaomba majukumu zaidi kwa mkuu wako pale unapoona majukumu uliyonayo ni madogo jitume sana na fanya mambo mengi,kama kuna watu wanakupigia simu waambie upo kazini na utawatafuta baada ya muda wa kazi!
👉🏻Uwe mtu wa matendo zaidi halafu pia hakikisha ukisema jambo unalifanya anza kufanya hata kama wengine bado hawaja anza,kitabu cha Bwana Larry Bossid kiitwacho Execution,aliandika kwamba watu wenye thamani kubwa na wafanyabiashara wakubwa wachache aliokutana nao walikuwa na tabia ya kuhakikisha kwamba wanafanya wajibu wao na wali hakikisha wafanya mambo au kazi wanazopanga!
👉🏻Ukweli ni kwamba utekelezaji wa wajibu kwa watu au kundi fulani la watu imeonekana kuwa ni sababu tosha ya mafanikio kwa mtu au taasisi fulani!
👉🏻Usipoteze muda fanyakazi muda mrefu zaidi punguzu muda wa kupoteza kuongea na wafanyakazi wenzako au kupokea simu zisizo za msingi au ambazo hazi husia na kazi unayoifanya kwa wakati huo!
👉🏻Kutokana na Robert half international,waajiriwa walio wengi huwa wanafanya kazi wastani wa 50% wa muda wao wa kazi,kwa hiyo 50% ya muda wao wa kazi hupotea kwa kuchelewa kazini,kuongea na wafanyakazi wenzao,wakati wakula chakula cha mchana au chai asubuhi na muda mwingine hupotea kwa matumizi ya simu na mitandao.
Wafanyakazi wanalipwa kwa 50% ya muda wao wa wakazi!
👉🏻Jenga tabia ya kufanya kazi kwa juhudi,imeonesha kwamba watu wengi waliofanikiwa kwenye mashindano ya mbio,wajasiliamali na matajiri binafsi wanajituma kufanya kazi ndio maana wamefanikiwa zaidi
👉🏻Katika utafiti uliofanyika nchini Marekani umeonyesha kwamba watu wanolipwa kidogo wanafanya kazi masaa machache ambayo ni masaa 25 kwa wiki ukilinganisha na hawa wanaolipwa kiasi kikubwa wao wanafanyakazi masaa 60 kwa wiki,kutokana na utafiti huu umeonesha kwamba kuna uhusiano wa moja kwa moja kwamba mtu anayefanya kazi kwa muda mrefu analipwa zaidi kuliko anayefanya kazi kidogo!

 VITU VITAKAVYO KUSAIDIA KUFANIKIWA KATIKA KAZI YAKO
👉🏻Andrew Grove mwenyekiti wa intel,alipo hojiwa na gazeti la fortune,kuhusu mabadiliko makubwa katika muongo mmoja uliopita,alisema kwamba kuna mambo mawili aliyoyaona ni kwamba,
      👂🏼 Kwanza,kila mmoja ni mbunifu wa maisha yake ni kwamba kila mmoja anawajibu wa mambo yanayotokea kwenye maisha yake kuhusu na tabia zake na maendeleo yake.
      👂🏼Pili,Kuongeza thamani ni muhimu sana kwa dunia ya leo,anasema siku za leo hata unapotaka ajira mwajiri huwa anaangalia utamwongezea thamani gani kwake kwa hiyo ni muhimu kuongeza thamani.
👉🏻Tabia za kuwa na maono ya maisha yako yajayo baada ya miaka 3--5 ni muhimu ili kujua unahitaji ujuzi gani ili uweze kuenenda na wakati na kufanikiwa zaidi.
👉🏻Peter Drucker aliandika ujuzi pekee katika karne ya 21 ni ujuzi wa kujifunza ujuzi mpya kwa sababu vitu vingi vinapitwa na wakati,ukweli ni kwamba chochote unachokifanya siku ya leo siyo ndio kitakacho kufanya ufikie malengo kuna ujuzi lazima ujifunze zaidi,Usisahau kwamba wewe unatakiwa kujifunza kila siku.
👉🏻Jenga tabia ya kujiona mshindi vaaa kama mtun anayejua aendako ktk maisha yake
👉🏻Ukweli ni kwamba watu wengi huvutia kutokana na mvuto wa nje na mwonekano wao katika sekunde 30 za mwanzo pindi mtu mwingine anapo muona,pamoja na kwamba kuna usemi usemao kwamba usimfikiria mtu kutokana na muonekano wake wa nje,ukweli ndio huo mvuto ni wa muhimu sana!
👉🏻Makapuni yaliyo mengi yanahitaji wafanyakazi watakakao endana na sare zao na mvuto kwa wateja wao wakati wa kutoa Huduma za kampuni hizo!jiulize je watu wanakuonaje ,umefananaje ,wanakutazama kama mtu mwenye mipango!?
👉🏻Jenga tabia ya kuzungumza lugha nzuri pindi unapokuwa na huduma maana maneno yanaweza kumuelezea mtu na tabia yake!
👉🏻Jenga tabia ya kuungana na wenzako na kufanya kazi katika makundi hii itakusaidia wewe kuongeza ujuzi  mbalimbali kutoka kwa wengine na kuongeza uzalishaji wako na jinsi gani uta muhudumia mteja wako!
👉🏻Jenga tabia nzuri za kuhudumia mteja wako,Tazama zaidi kwenye huduma zako kwa mteja wako,jarbu kuona kila mtu kwako ni mteja na wewe ni mbobezi wa kutoa huduma kwa mteja wako,
 Maana ya mteja Mtu yeyote ambaye una mtegemea katika mafanikio ya kazi au biashara yako au mtu yeyote yule anayekutegemea kufanikiwa kwenye maisha yake!
👉🏻Kutoka na maana hiyo hapo juu tuna aina mbili za wateja,
  🔥kwanza,mteja wa nje,huwa ni watu wanokuja kununua zao lako au huduma yako,unapowaridhisha wateja hawa basi huwa inakuwa ni mafanikio makubwa kwako ni watu muhimu sana kwenye biashara yako au kampuni yako!
   🔥Pili,Mteja wa ndani,huwa ni wafanyakazi wenzako hususani hawa huwa kwenye kampuni au benki unapowaheshimu na kuwafanyia yaliyo mema basi pia huleta mafanikio katika ile kazi yako mwenyewe!
👉🏻Mteja wako maalumu kwa wale wafanyakazi ni yule mkuu wako ukimridhisha mkuu wako na wafanyakazi wengine unajitengenezea mahali pazuri na mazingira ya mafanikio ya biashara yako! Siku zote mweke mkuu wako kama wa kwanza.
👉🏻Jenga tabia ya kusaidia wafanyakazi wengine kama wakiwa na uhitaji hii itakujengea wewe kuwa mmbobezi mzuri kwa wateja wa ndani maana yake wafanyakazi wenzako.
👉🏻Unapokuwa unafanya kazi za watu jione kama wewe ndio bosi wa ile kazi au umejiali na unahitaji kazi yako ifanyike kwa ufasaha zaidi na ifanyike kwa 100%,unapokuwa unaona kama kazi ile ni yako itakusaidia kuchukua wajibu wako asilimia mia moja.
👉🏻Katika utafiti uliofanyika New york waligundua kwamba 3% ya wafanyakazi ndio huwa wanafanya kazi za watu kama zao yani kama wamejiari na ndio wao huwa maarufu na wanalipwa vizuri ukilinganisha na kundi lilobaki,kwa sababu wao hujituma na kutimiza wajibu wao kwa wakati.
👉🏻 Jenga tabia ya kuona kila mtu kwa upande mzuri,yani kumuona mwenzako chanya pamoja na kwamba atakuwa ana madhaifu,na ujenge tabia ya kuwa fikiria watu wanaokuzunguka wala usiwachukie na kuwasema vibaya pale wanapokosea,tabia hii ni nzuri kwa sababu utawasaidia wenzako na kuongeza thamani ya huduma kwa wateja au thamani ya kampuni .
👉🏻Make it a habit to look for the good in every person and situation!,
            

                                            DEVELOP YOUR GOOD HABITS

                                               SURA YA SABA,

             TABIA ZA WAFANYABIASHARA WAKUBWA,

👉🏻Bwana James Whitcomb Riley aliwahi kusema kwamba mtu anayendelea kupambana na kujituma pamoja na kwamba jitihada hizo hazionekani kwa watu na mtu akijituma bila kukata tamaa na kujitambua vema mwisho wa siku mtu huyo atafanikiwa wala asivunjeke moyo.

👉🏻Kitu chochote ambacho hutokea kwenye maisha hutokea kwa sababu ya uwezekano tu,kuna uwezekano kwamba utaishi maisha marefu,utakuwa na afya njema na nk,kuna uwezakano kwamba kesho utaamka na utaenda kazini salama!

👉🏻Unapokuwa una ujuzi na elimu ya kutosha kuhusu kufanya biashara vizuri basi huwa kuna uwezekano mkubwa utapata faida kubwa au kupata fedha nyingi na pia kuna uwezekano mkubwa kwamba utakuwa huru kifedha na kuwa milionea miaka ijayo.

👉🏻Kama ilivyo kwenye ujuzi mwingine,ujuzi katika biashara huja kwa kujifunza ujuzi wa biashara na kwa kufanya jambo ulilojifunza katika biashara yako!

👉🏻 Lengo la biashara au kazi ya biashara,Baadhi ya watu wanasema lengo la biashara ni kutengeneza faida lakini Bwana Peter Drucker alisema kwamba lengo la biashara ni kutengeneza na kuwabakisha wateja katika biashara yako, Ni kwamba faida unayoipata kwenye biashara yako ni kutokana na wale wateja uliowatengeneza na kuwasaidia wateja na hapo ndipo unapata faida!

👉🏻Moja wapo ya tabia muhimu za kuzijenga ni *tabia ya kumfikiria mteja wako muda mrefu
Hakikisha kwamba unamlenga mteja muda wako wote kuanzia asubuhi mpaka jioni!

👉🏻 Lengo la biashara ni kumridhisha mteja* Biashara hufanikiwa na kukua zaidi pale ambapo wateja wanaridhika vema na huduma yako ukilinganisha na wale washindani wako.Biashara hushindwa kukua na kuendelea kutokana na kushindwa kuwaridhisha wateja inawezekana kwa sababu ya zao lako,huduma yako na bei yako ya vitu unavyo uza.Ili kujua kwamba huduma unayotoa kwa wateja ni sahihi ni muhimu kujiuliza swali kwamba je mteja wako anataka nini au thamani gani anahitaji mteja wako!?

👉🏻Mojawapo ya mambo ya muhimu katika biashara yako au mafanikio ni kuweka wazi na kuwa mkweli kwamba wewe ni nani na unafanya nini katika biashara yako au kazi yako.Lazima ujenge tabia ya kufikiri kwa makini katika kila mipango ya biashara yako na tumia muda fulani ili kutekeleza maamuzi yako katika kila eneo mfano hii ni katika biashara yako maana yake katika kila eneo la biashara yako!

👉🏻Anza na maono yako,Je maono yako katika biashara ni nini!?Kama unataka uje kuwa mfanyabiashara mkubwa,Je unataka biashara hiyo utataka iwe ina muonekano gani!?.Biblia inasema kwamba Pale pasipo na maono basi wanadamu hupotea,maana yake ni kwamba ikionekana kama hakuna uhakika na ukweli wa mambo yajayo watu hukosa uaminifu na watu hupoteza matumaini katika lile ambalo walitegemea kulifanya wakati ujao!

👉🏻Fikiria pia kuhusu je maneno unayotumia kuelezea biashara yako je ni maneno yenye mvuto kwa wateja wako,unatumia maneno gani ili kuelezea biashara yako na kuvuta wateja kwenye biashara yako!

👉🏻Ni muhimu kujua kazi kubwa ya biashara yako ni nini!?je kazi kubwa ya biashara yako ni nini?

👉🏻Lazima kujua ni kusudi gani la biashara yako?,Unapoweza kusema au kutambua kusudi la biashara yako basi utaweza kupata jibu kwa nini unafanya biashara katika eneo fulani?

👉🏻Ukiwa umeelewa kazi,maono na kusudi la biashara yako, unatakiwa kuweka mambo hayo katika mfumo wa kupimika na muda maalum na malengo  ya biashara yako na malengo yako yagawanyike kwa mfumo wa muda mrefu,wakati na muda mdogo!,Unahitaji malengo kuhusu kiasi gani umelenga kuuza na kiasi gani unahitaji kupata katika hayo mauzo yako,Unahitaji malengo yako ya maendeleo na uingizaji wa zao na huduma mpya na uendelezaji wa zile huduma za zamani.

👉🏻Drucker alisema kwamba kazi kubwa ya meneja ni kuwa mbunifu na kutafuta masoko ya biashara kwa sababu kwenye biashara kuna kazi mbili muhimu kutengeneza na kuwabakisha wateja katika biashara yako hapo ndipo utapata matokeo ya kifedha.

👉🏻Siku zote mteja ni mfalme,mteja anahitaji kitu kimoja tuu ambacho ni uboreshwaji wa huduma ya biashara yako Sababu kubwa mteja ananunua kitu kwenye biashara yako ni kwa sababu anataka kuboresha maisha yake!,mteje siku zote yupo sahihi!

👉🏻Mtaje siku zote ni mbinafsi,kwa sababu mteja anahitaji kupata kikubwa kutoka kwenye kidogo alichonacho yeye,anahitaji huduma bora kwa gharama ndogo,wateja wanahitaji kitu chochote kizuri,haraka,bei poa na rahisi kununua na kutumia hiyo bidhaa yako!.

👉🏻Ni muhimu kujenga tabia ya kuboresha huduma yako mara kwa mara, na mojawapo ya sababu kubwa za kufanikiwa kwa wafanyabiashara wakubwa na wajasiliamali ni kwa sababu wamejikita zaidi kuangalia masoko na kuwajali wateja wao.


👉🏻Jenga tabia ya kifikiri kama mjasiliamali,kwa kawaida mjasiliamali ana mambo mawili huwa anayafikiria ambayo ni
 ❤ Kwanza,Uharaka, wajasiliamali wanatabia ya kuchangamkia furusa mapema na kuzitendea kazi haraka iwezekanavyo au kutatua tatizo mapema,Siku hizi jambo la muda ni muhimu sana kwenye jamii,kama utaweza kutoa huduma kwa muda mwafaka utavutia wateja wako katika biashara yako.
 ❤ Pili,kubadilika kutokana na mazingira, ukweli ni kwamba wajasiliamali hubadilika na kujifunza kutokana na mazingira na muda unavyokwenda.

 TABIA SABA ZA KUKUFANYA UFANIKIWE KATIKA BIASHARA YAKO

👂🏼 Kwanza,Tabia ya kupanga kuhusu biashara ni muhimu kuwa na mpamgo biashara katika biashara yako unayofanya,unapokuwa na mpango biashara mzuri ni rahisi kufanya biashara yako, unapotumia muda wako 20% kupanga biashara yako basi utakuwa  umetunza muda wako kwa 80% kwa ajili ya kufanya mambo mengine katika biashara!

👂🏼 Pili,Jenga tabia ya kupangilia watu gani au wafanyakazi gani na malighafi za kutumia kabla hujaanza kufanya biashara yako, unafanya hivyo unapangilia kwa pamoja wale watu unaowahitaji na zile malighafi katika mpango wako wa biashara.

👂🏼Tatu,Jenga tabia ya kuajili watu sahihi katika biashara yako, 95% ya mafanikio ya wafanyabiashara wakubwa na wajasiliamali wakubwa ni kutokana na kuajili watu sahihi katika biashara zao.

👂🏼 Nne,Jenga tabia ya kugawanya kazi vizuri, unapofanya mgawanyo wa kazi vizuri kwa wafanyakazi wa biashara yako inakusaidia wewe kuendesha vema biashara yako!Wape uhuru wafanyakazi wako hakikisha wanakuwa huru na wanafanyakazi wenyewe bila ya nguvu nyingi kutoka kwako!

👂🏼 Tano,Jenga tabia ya kuwa msimamizi mzuri ,baada ya kugawanya kazi vizuri hakikisha unasimamia vema majukumu ya kila mfanyakazi,kumbuka unapoendelea kugawanya kazi na kusimamia vema ndivyo utavyofanikiwa katika biashara yako!

👂🏼 Sita , Jenga tabia ya kupima ufanyajikazi wenu katika biashara ,hakikisha unajenga tabia ya kujitathimi katika ufanyaji kazi wa biashara yako!

👂🏼 Saba,Jenga tabia ya kupata matokeo mara kwa mara unapojitathimini kuhusu ufanyaji wa biashara yako hakikisha unakuwa na utaratibu maalum kila mfanyakazi au mteja anatoa mawazo yake katika biashara yako kuhusu maendeleo na huduma za biashara yako!
TABIA ZA WASHINDI KATIKA MASUALA YA BIASHARA,

👉🏻Mojawapo za tabia za wafanyabiashara wakubwa ni kutambua kuwa wao wanatakiwa kushinda,kufanikiwa na kuwazidi washindani wao ili kufanikiwa katika biashara zao.

👉🏻Tabia nyingine ambazo watu wakubwa wanazo ni kujiuliza na kuwa nadhana fulani endepo wafashindwa kufanya biashara yao vizuri na hapa hujiuliza maswali mengi mfano,Ukweli kuhusu biashara,masoko,wateja,mazao nk

👉🏻Tabia nyingine ambazo watu wakubwa wanazo ni kufiri kabla ya kutenda mambo,kuna sheria inasema kwamba kama maamuzi hayakufanywa kwa wakati fulani,haifai kufanya hayo,jenga tabia ya kujiuliza maswali mengi kabla ya kufanya jambo fulani!

👉🏻Watu wakubwa na wafanyabiashara wakubwa huwa wanatabia ya kuwa na kundi fulani (mastermind group), ambapo huwa wanajifunza mambo ya biashara na kujuzana kuhusu changamoto za biashara zao na masoko pia!

👉🏻Wafanyabiashara wakubwa huwa wanatabia ya kufikiri zaidi kuhusu uzalishaji wao na uzalishaji wa biashara zao,wanaangalia njia za kupata kingi kupitia vitu vidogo walivyo navyo na kwa gharama ndogo.

👉🏻Wafanyabiashara wakubwa huwa wanatabia ya kufikiri kuhusu jinsi gani watawaridhisha wateja wao,na hapa ndipo hujua kwamba wateja wao wanahitaji nini katika biashara zao, Bwana Thomas Monaham,mwanjilishi wa Domino's pizza alisema kwamba kwa upande wake kwamba wateja wanarihika kutoka na uharaka wa kuleta huduma kwao kwa sababu wateja wanapotaka pizza huwa wananjaa wanahitaji kula bila kuangalia ubora au gharama ya hiyo pizza!
Inategemeana kuna wateja wengine unapojali muda basi wao ndio wanaridhika, je wateja wako wanataka nini ili waridhike na hiko kitu hawapati kwa washindani wako!?

👉🏻Wafanyabiashara wakubwa huwa wanatabia ya kufikiri kuhusu faida wanayopata kutoka kwenye huduma wanazotoa kwa wateja wao,wafanyabiashara walio wengi wamejikuta ndio wanawateja wengi lakini hawana faida na kama wanapata faida basi ni faida ndogo sana na kwa sababu pia hawajui gharama fulani za biashara zao ambazo zimejificha!

👉🏻Wafanyabiashara wakubwa huwa wanatabia ya kufikiri kuhusu ubora wa huduma zao kwa wateja wao muda wote,ni muhimu kuboresha huduma zako kwa mteja kwa sababu mteja anapokuja kwako anafikiri kwamba huduma yako ni bora kuliko ya washindani wako!

👉🏻Wafanyabiashara wakubwa huwa wanatabia ya kufikiri kuhusu kuwajenga watu( wafanyakazi) na kutunza muda,wafanyabiashara wakubwa wanajenga tabia ya kuwafundisha na kuwa ruhusu wafanyakazi wao kuhudhuria semina  mbalimbali kwa ajili ya kujifunza mambo ili kuboresha huduma kwa wateja wao.

👉🏻wafanyabiashara wakubwa huwa wanatabia ya kuongoza vyema biashara zao,jenga tabia ya kuongoza vema biashara yako!

👉🏻Wafanyabiashara wakubwa huwa hawaridhiki na huduma huwa ni wabunifu siku zote za maisha yao na huwa wanatabia ya kuhamasisha ubunifu kwa wafanyakazi wao na kufanya mijadala kwa ajili ya kuboresha huduma zao pamoja na kuwapa zawadi wale wafanyakazi wanaotoa mawazo mazuri ili kuboresha biashara zao.

👉🏻KUMBUKA HAKUNA KAMA WEWE DUNIANI NA HAKUNA ALIYE BORA ZAIDI YAKO,KAMA KUNA MTU NI BORA ZAIDI YAKO LEO JUA KWAMBA ALIJENGA TABIA FULANI KABLA WEWE HUJAKUWA NA TABIA HIYO,HIVYO BASI WEWE PIA UNAWEZA KUWA BORA ZAIDI KAMA TU UTAJITUMA KUJIFUNZA TABIA ZA MAFANIKIO

👉🏻Six P acronym that says," P roper P rior P lanning P revents P oor P erformance!,
         DEVELOP YOUR GOOD HABITS
          Ahsante,
  Usikose kesho sura ya nane ya kitabu,
     Phone.0742364499,
Email.mwanyikajackson428@gmail.com


No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]