Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]


            *TWO MEN ~ ONE MESSAGE*
.Tokeo la picha la WHY WE WANT YOU TO BE RICH by DONALD J. TRUMP & ROBERT T.KIYOSAKI.
             SEHEMU YA TATU

                     *SURA YA ISHIRINI*
JE FALSAFA YAKO NINI KUHUSU MASUALA YA MUNGU,DINI NA FEDHA?.
👉🏻Mwandishi wetu KIYOSAKI anasema kuna vitu vilikuwa vinamchanganya kuhusu MUNGU, kanisa la kweli na Dini ya kweli.

👉🏻Anasema wazo la kwanza ilikuwa ni kwamba kuna watu watakwenda mbinguni na wengine watabaki yani hawataenda hata kama wana amini katika MUNGU mmoja.

👉🏻Anasema siku moja alimuuliza mwalimu wake wa shule ya jumapili kwamba kuna utofauti gani kati ya kanisa alikokuwa ana sali na kanisa la kikatoliki wakati anamuuliza alikuwa ana miaka 8 na anasema badae mwalimu wake alimuchanganya baada ya kusema watu wengine wataenda mbinguni isipokuwa wakatoliki hawata enda pamoja na kwamba wote wana amini kwa Yesu kristo.

👉🏻Na baadae akauliza vizuri kwa Mwalimu wake ndipo akasema kwamba kanisa la wakatoliki si kanisa la kweli!,

👉🏻Anasema baada ya muda kidogo akawaambia na akawaomba marafiki zake wakatoliki waende kusali pamoja ndipo walipofika kanisani na wakapongezwa kwamba wako sehemu sahihi na wanaamini MUNGU yule yule mmoja ndipo KIYOSAKI akaacha kwenda kanisani kwao yani kwa wazazi wake na akamuuliza Mama yake na  Baba yake kwamba je kunatofauti kati ya wao na wale wakatoliki na wazazi walikubali kwamba utofauti upo.

👉🏻Anasema baada ya miaka kadhaa kupita akahudhulia makanisa mbalimbali ya marafiki zake ingawa anasema alikuwa hana rafiki Myahudi na Muislamu na akaona kila kanisani au dhehebu na Dini wao wanajiona wako sahihi kuliko upande mwingine, anasema kiukweli watu wapo huru kuchagua mahali pa kusalia lakini kinachoshangaza wale ambao wanasema wako sahihi sana kuliko wengine na kuwaambia kwamba hawata enda Mbinguni na kuna dhehebu au Dini moja tu ndiyo ya kweli na hii ndio kisababishi kikubwa cha vurugu,vita na migogoro katika jamii kutokana na MUNGU na Dini.

👉🏻Anasema yeye ana amini katika MUNGU kwa sababu wakati yupo kwenye vita kule Vietnam ameshuhudia vifo vikubwa vya marafiki zake na yeye akawa mzima mpaka leo.

👉🏻Anasema katika masuala ya biashara kwamba lazima atimize malengo na maono makubwa aliyokuwa nayo na aliyojipangia na hii kwa sababu anamini MUNGU yupo na ndio maana hafanyi biashara kiujanja janja na anafanya kwa maadili ambayo hata MUNGU anaruhusu tofauti na dhuruma.

👉🏻 *Sheria ya muhimu kwa watu wote Wafanyie wenzako kadiri wewe unavyopenda wakufanyie,*
 Mfano umemkosea rafiki yako ni vema kumwita na kumwomba msamaha mapema siyo mpaka yeye akuanze eti kwa sababu wewe una kitu fulani au uko na nafasi fulani hiyo ni tabia ya ukaidi haifai.

👉🏻Tafuta sehemu sahihi ya kuabudia na uwe na maisha yako binafsi, Mwandishi anasema anapenda Dini ya Wahindi inaitwa DHARMA ambayo ina maana kwamba fuata chaguo lako la sehemu ya kuabudia bila kufuatilia Dini za wenzako.

👉🏻Kitu kingine kilichomchanganya bwana KIYOSAKI ni kuhusu fedha na MUNGU, anamkumbuka Rafiki yake mama yake alikuwa ni tajiri na alikuwa anasema kwamba Fedha ina leta mambo mabaya Duniani, anasema alimshangaa yule Mama kwa nini kama Fedha ni Adui kwa jamii asipeleke kanisani abaki hivi hivi.

👉🏻Anasema yeye KIYOSAKI hafikirii kwamba watu matajiri ni wapinga kristo na pia anashangaa eti kweli kwamba Masikini wataenda mbinguni harafu Matajiri watabaki.

👉🏻KIYOSAKI anasema siku moja aliuliza swali kwa viongozi wake wa kanisani kuhusu masuala ya fedha ndipo majibu yalikuwa hivi.

📌Jibu la kwanza ni kutoka kwa kiongozi wa zamani ambapo alisema Mtu akipenda fedha itakuwa ni mzizi wa kufanya mambo mabaya na akaongeza kwa kusema ni Rahisi kwa Ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kwenda Mbinguni.

📌Pili alikuwa ni kiongozi kijana ambaye yeye kabla ya kusema kuhusu kupenda fedha alitoa ile historia ya kwenye kitabu cha Mathayo Kuhusu talanta ambapo yule Tajiri kabla hajaondoka kwenda safarini aliwapatia watumishi wake watatu talanta kama ifuatavyo!

💥Yule wa kwanza alimupa talanta tano baada ya tajiri kurudi yule mtumishi alikuwa amezalisha mara mbili zaidi zikawa kumi.

💥Yule wa pili alimpa talanta mbili ambapo naye akazilisha mbili zaidi zikawa nne.

💥Yule wa tatu alipewa moja akachimba shimo na kafukia hakuzalisha maana yake.

👉🏻Tajiri alipo rudi aliwa sifia kwa uaminifu wale watumishi wa wili wa kwanza . Anasema badae yule kiongozi kijana akawaambia unafikiri yule tajiri alikuwa ana maana gani?

👉🏻Ndipo Binti mmoja Mdogo akasema yule tajiri alikuwa anataka watumishi wake na sisi pia tuwe matajiri na tajiri atakuwa na furaha kuona watumishi wake wanakuwa matajiri kama yeye!

👉🏻Kiongozi kijana akasema jibu alilojibu Binti siyo jibu sahihi akamalizia kwa kusema ile stori ya yule mtumishi wa tatu ambapo tajiri alipo muuliza kwa nini hukuzalisha yeye alisema alifukia alikuwa anaogopa kuibiwa ili tajiri aje aikute iko salama,lakini tajiri alimwambia mtumishi yule kwamba hana maadili na amekuwa siyo mwaminifu,na aliwapongeza sana wale wa kwanza kiukweli shule ya kiongozi ilikuwa ni njema sana.


👉🏻Je vipi wewe falsafa yako kuhusu MUNGU na Dini ikoje??
_________________________________________________

👉🏻Je  masuala ya kifedha yana athiriwaje na imani yako?
_________________________________________________

👉🏻Our main Job is to make life here on earth a little bit more like heaven.



                      YOU MUST BECOME A RICH
                      Ahsante,
     Usikose kesho sura ya ishirini na moja ya kitabu.
                     Phone.0742364499.
      Email.mwanyikajackson428@gmail.com
.


No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]