Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]

 Tokeo la picha la INTERACTION TOWARD SUCCESS
1/3: Katika kitabu  cha TABIA 12 ZINAZOLETA MAFANIKIO nimeeleza TABIA 12 muhimu katika zile 300 ambazo kwa mujibu wa Tim Corley ndizo hasa zinafofautisha matajiri na maskini,Hii ni baada ya Tim kufanya utafiti kwa Muda wa miaka 5 kwa matajiri 233 na maskini 128.
.
TABIA YA 01: Ni kuwa na mwelekeo ambao Uko dhahiri sana (Clarity of Purpose).Hii inamaanisha hautakiwi kuamka kila siku na kuanza kukimbizana na maisha bali kila unachofanya kichangie katika mwelekeo wa Maisha Yako.
.
Moja ya changamoto ya watu wengi ni kuwa bize ila kukosa mwelekeo unaoeleweka,wengi wanashindwa kutofautisha kati ya “KUENDELEA MBELE NA KUTEMBEA TEMBEA”(Progress VS Movement).
.
Kwa Mujibu wa Prof:Edwin Locke na Dr.Gary Latham katika utafiti wao wa miaka 8(1960-1968) walionyesa kuwa mtu ambaye ameshajua anakoelekea ana uwezekano mkubwa wa kufanikiwa na anakuwa na hamasa zaidi ya Maisha kuliko mwingine.
.
Je,wewe umeshajua bidii yote unayofanya unaelekea wapi?(Clarity of Purpose).


 2/3: Tabia ya pili zilizoeleza katika kitabu cha TABIA 12 ZINAZOLETA MAFANIKIO ni KUJIAMINI katika maisha Yako.Kuna watu wengi sana wanafeli sio kwa sababu hawana uwezo au hawapati fursa ila hawajiamini kabisa katika maisha yao.Kuna watu hawaamini kama wanaweza kufanikiwa,wengine ni waoga hata kusema mawazo yao au kusimama mbele za watu tu kuongea.
.
Hofu husababishwa na mambo mengi ya kisaikolojia,kihistoria na hata kibaiolojia.Kutokujiamini hutokana hasa na namna unavyojiona “self-concept”.Hii hutokana na Maneno uliyowahi kuambiwa,Mambo uliyopitia na hata kama uliwahi kufeli huko nyuma.
.
Kwenye Maisha ya watu wengi kuna viwango ambavyo wamejiwekea kuwa hawawezi kabisa kuvifikia (Self-Limiting belief).Kuna watu hawaamini kama wanaweza kufanikiwa zaidi ya sasa,kuna watu wanaamini maisha duni au matatizo waliyonayo yatadumu nao milele.Kuna watu hadi wanasema “Mi ndio niliumbiwa haya”.Watu waliofanikiwa wanajiamini sana,wanaamini uwezo wao,ndoto zao na wanaamini kupata mabadiliko.

Je,una kuna eneo la Maisha yako unahitaji kujenga hali ya kujiamini?


3/3:Tabia ya tatu iliyoelezwa katika Kitabu cha TABIA 12 ZINAZOLETA MAFANIKIO ni kuanza na kidogo ulichonacho.
.
Mwaka 1886 mfamasia John Pemberton ambaye kwa wakati huo alikuwa anajulikana kwa jina maarufu la Mr.Doc alikuwa amerudi kutoka vitani na akawa anawaza kujaribu tena baada ya kufeli mara kadhaa alitaka kugundua Kitu kitakachompa faida ya kibiashara.
.
Baada ya kufanya majaribio ndipo aligundua “formula” ya kikemikali ya kutengeneza kinywaji cha Coca-Cola na kwa kushirikiana na Frank Robinson walitengeneza logo na Kauli mbiu ya kwanza ya Coca-Cola ya “The Pause That Refreshes”.
.
Hata hivyo kwa mwaka mzima wa kwanza walifanikiwa kuuza chupa 25 tu ingawa kwa sasa wanauza zaidi ya chupa billioni 1.8 kwa Mwaka.
.
Kanuni ya kuanza kidogo unaweza kuitumia kwenye Fedha,biashara na hata kazi unayofanya.Badala ya kudharau kidogo ulichonacho,jiulize:NITATUMIAJE KIDOGO NILICHONACHO KUPATA KIKUBWA NINACHOKITAFUTA?Je,wewe una Nini kidogo leo ambacho unaweza kuanza kukitumia?
.
Kwenye kitabu hiki cha TABIA 12 ZINAZOLETA MAFANIKIO nimeeleza pia unavyoweza kupanga mpango wa kujipatia uhuru wa kifedha kwa kuanza na pesa,mtaji au kazi ndogo uliyonayo.





No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]