Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]

 Tokeo la picha la the best way to start is to start
Gil Penchina aliwahi kusema-“Momentum Begets Momentum,and the best way to start is to start”(Unapoanza mwendo unapata nguvu za kuendelea mbele zaidi na Njia nzuri ya kuanza ni kuanza).
.
Moja ya Uongo mkubwa sana ambao watu huwa wanajiambia ni kuwa HAWAKO TAYARI BADO KUANZA,Ngoja NISUBIRIE Kuishi Ndoto yangu nitaanza KESHO nikiwa tayari.Kuna ndoto nyingi sana huwa zinakufa kwa sababu ya watu kuamini kuwa hawako tayari leo kufanya kile ambacho wanatamani kukifanya.
.
Unaposoma ujumbe huu najua moyo na akili yako inakukumbusha jambo ambalo ulipanga kulifanya Mwaka huu na hadi leo haujalifanya kwa sababu unasema “naona bado siko tayari”.
.
Kumbuka kuwa kufanya mambo Makubwa kwenye maisha huwa hakuendani na kujisikia kwako kama Uko tayari bali kunatokana na KUAMUA KUWA TAYARI.
.
Usiendelee kusubiria kujisikia kuwa tayari kuanza biashara,AMUA KUANZA LEO,usisubiri kujisikia kuwa tayari kuchukua maamuzi,AMUA KUCHUKUA MAAMUZI LEO,Usisubirie ujisikie kufanyia kazi wazo lako,AMUA KULIFANYIA KAZI LEO,Usisubirie kujisikia kubadilisha unachofanya,AMUA KUBADILISHA.
.
Ukianza kuchukua hatua moja leo bila kujali ni ndogo kiasi gani,itakupeleka nguvu ya Kuchukua hatua zinazofuata.JE,UKO TAYARI au bado UNASUBIRIA ujisikie kufanya?Mimi Niko tayari.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]