Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]


TWO MEN ~ ONE MESSAGE
.Tokeo la picha la WHY WE WANT YOU TO BE RICH by DONALD J. TRUMP & ROBERT T.KIYOSAKI.
           SEHEMU YA NNE

        SURA YA ISHIRINI NA MBILI

MIMI NI MZEE SINA FEDHA ZA KUTOSHA KUENDESHA MAISHA YANGU JE NINATAKIWA KUFANYA NINI?
👉🏻Mwandishi anasema kwa kizazi cha wazazi wetu na mababu zetu yani kizazi kile cha wakati wa vita ya pili ya Dunia, sheria za mafanikio zilikiwa rahisi kwamba mtu anaenda shule,anapata kazi ambapo serikali au kampuni fulani ina mlinda kiafya hata kama mtu huyo ataingia uzeeni na kustaafu kazi hiyo.

👉🏻Lakini katika Dunia ya leo hii sheria imebadilika kabisa na mabadiliko yalianza mwaka 1971 ambapo dollar ilibadilika na kuwa sarafu inayotembea kutoka sehemu moja hadi nyingine, maana yake ni kwamba serikali inaweza kuzitengeneza nyingi zaidi kuliko kuitunza sehemu moja.

👉🏻Mabadiliko mengine ilikuwa ni mwaka 1974,ambapo makapuni yaliacha kuwalinda waajiliwa katika masuala ya afya kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

👉🏻Bado pia kuna mabadiliko kwamba kumekuwa hakuna ajira na hata kama ajira zipo bado mshahara haukidhi mahitaji ya waajiliwa,Bado kuna waajiliwa wao wanasema kwamba wanalindwa na serikali mfano Mwalimu,Daktari na nk lakini wakumbuke kazi hizo miaka ya leo zina ushindani mkubwa sana.

URAHISI AU UGUMU
👉🏻Mwandishi anasema kama wewe ni mzee au mtu mzima sana kuna vitu muhimu viwili ambavyo unapaswa kuchagua ambavyo ni;

📌Kwanza, Uishi chini ya viwango.

Au

📌Pili,Upanue viwango vyako vya kimaisha.

👉🏻Kwa maana nyingine ina maana chagua kuishi;

📌Kirahisi.

Au

📌Kigumu.

👉🏻Mwandishi anasema alikuwa na marafiki ambao walikuwa wanaishi chini ya viwango vyao na walikuwa wanaishi maisha ya furaha.
Maana yake walikuwa wanaishi kirahisi.

👉🏻Anasema wao na DONALD wanafanya biashara sehemu yoyote Duniani wanayoipenda masaa 24 siku 7 za wiki,wanafanya biashara kila sehemu kwa kusafiri sana na wana majumba sehemu kubwa huko Marekani.

👉🏻ROBERT anasema yeye na mke wake Kim wanamarafiki katika Dunia nzima na namna ya maisha yao inawasaidia kuwa na mahusiano ya muda mrefu na watu dunia nzima katika biashara na kibinafsi wao kama familia.




👉🏻Mwandishi anasema kwamba sababu muhimu za kusema mtu anatakiwa kuchagua kuishi kigumu au kirahisi au namna zote mbili kwa pamoja hii ni kwa sababu chaguzi zote zinahitaji muda,fedha na mipango.

👉🏻Mtu mzima ni muhimu kujua unapenda namna ipi uishi kwa sababu hakuna namna ambayo ni mbaya au nzuri kupita nyingine, Kwa hiyo cha muhimu fanya mipango maalum sasa kabla hujachelewa sana,maisha ni mafupi sana na kuna mambo muhimu zaidi ya fedha.

👉🏻Kama utataka kuishi maisha ya raha kwa kuwa na uhuru wa kifedha basi ni muhimu kupanua viwango vya kifedha,na kwa kuongeza ugumu wa namna ya kuishi maana yake ni kwamba unaongeza uelewa kuhusu masuala ya fedha katika ulimwengu wako unaokuzunguka na ulimwengu wa watu wengine.

👉🏻Pia kujua kuhusu masuala ya biashara katika Dunia nzima ni muhimu ili kujua kinaendelea nini katika nchi nyingine na hizi habari utapata kupitia kusoma magazeti na kusikiliza vyombo vya habari.

👉🏻Pia kuishi kigumu maana yake ni kukutana na kufanya biashara na watu tofauti tofauti. Katika ulimwengu wa ujasiliamali na wa watu wenye uwezo wa kuwekeza utakutana na watu wenye sifa ambao watakujenga na wewe katika masuala ya fedha.

👉🏻Pia kuishi kigumu kwa mashindano maana yake ni kwamba unakuwa mwanafunzi katika ulimwengu wa fedha,watu na biashara masaa 24,siku saba za wiki na wiki 52 za mwaka mzima. Katika mchezo wa fedha kama huna akili vizuri unaweza ukapata hasara ila kama uko vizuri kwenye elimu ya fedha basi fedha nyingi zitakuwa zinaingia kwako kama maji hivi.

👉🏻Katika dunia ya leo ni wewe tu kuchagua unataka kufanya biashara gani na katika nchi gani kwa hiyo tuko huru kwa sababu ya utandawazi unaweza ukawa kijijini tu sehemu fulani lakini ukafanya biashara sehemu kubwa duniani bila hata kusafiri una safiri kielektroniki tu kwa compyuta au simu yako tu.

👉🏻Kwa watu ambao hawana chochote harafu wanataka kuwa matajiri hebu fanya kitu cha nadhari kwamba unataka kushinda medali ya dhahabu katika mchezo kwenye Olympic ujao,kwa hiyo basi weka malengo yako sasa baada ya kuweka malengo jiulize swali kwamba
Olympic katika kipindi gani baridi au joto?

Swali la pili katika mchezo gani kuogelea,kukimbia nk?

👉🏻Baada ya kuchagua sehemu au mchezo unaoupenda,anza kujifunza,soma na tafuta kiongozi wako kama kocha akuongoze halafu jihakikishie na jitoe kushinda katika mchezo na kuchukua medali hiyo.

👉🏻Unapojihakikishia kushinda ni rahisi kushinda ila bila kujitolea kushinda nafasi ya kushinda mchezo na kuwa tajiri ni ngumu kwako.

👉🏻Tathimini kuhusu ukweli wako kwamba je katika utu uzima wako jiulize mwenyewe katika ukweli wako kwamba unakwenda na Dunia au dunia imekuacha nyuma.

👉🏻Kama uko tayari kujiunga kwenye utandawazi na kuishi kigumu fuata mambo ya fuatayo;

📌Tafuta marafiki wapya na wa zamani au jiunge kwenye club za watu wenye mawazo kama yako.

📌Safiri sana,jifunze na ukue baada ya kuona vingi duniani

📌Soma vitabu mfano

📒The world is Flat by Thomas Friedman
📒The Dollar Crisis by Richard Duncan
📒A Whole New Mind by Daniel Pink
📒The Coming Economic Collapse by Stephen Leeb
📒The America We Deserve by DONALD TRUMP




👉🏻Club ambazo unaweza kujiunga ziko za aina mbili ambazo ni;

📌Commercial CASHFLOW clubs hizi zinaundwa ambapo mwanzilishi anatumia CASHFLOW game kama njia ya kuelekeza kundi katika mchezo wa fedha lakini pia na zile bidha wanazo uza.

📌Educational CASHFLOW Clubs hizi zinaundwa kwa ajili ya kufundishana kwa marafiki na hata wana familia kuhusu masuala ya biashara na uwekezaji.

👉🏻Pia ni muhimu kujifunza kuhusu msingi wa uwekezaji na jinsi au mbinu za uwekezaji kwa kuata hiyo michezo ya CASHFLOW 101 na CASHFLOW 202 kwa kila mmoja

👉🏻DONALD anasema kwamba jitathimini ujuzi wako,kitu gani una Pendelea, sehemu uliyopo na weka akilini mwako halafu fanya mabadiliko katika maisha yako, yani fanya kama unaona fursa mpya na vitu vikubwa vitakuja kwako siyo kitu rahisi ila ukiwa unajihakikishia vitakuja tu.

👉🏻Vyovyote unavyofanya usikate tamaa,jitathimini unataka kufanya nini halafu hakikisha unafuata miongozo kufikia hiko unachotaka kwa wakati huo na kuweka visingizio vya kushindwa haitakiwi kabisa.

👉🏻Due to diligence equals increasing your financial IQ daily.


YOU MUST BECOME A RICH
Ahsante,
Usikose kesho sura ya ishirini na tatu ya kitabu.
Phone.0742364499.
Email.mwanyikajackson428@gmail.com.


No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]