Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]

WHY WE WANT YOU TO BE RICH by DONALD J. TRUMP & ROBERT T.KIYOSAKI.Tokeo la picha la WHY WE WANT YOU TO BE RICH by DONALD J. TRUMP & ROBERT T.KIYOSAKI.

         TWO MEN ~ ONE MESSAGE

               SEHEMU YA TATU

 SURA YA KUMI NA NNE
NI KITU GANI UNAJIFUNZA AU UMEJIFUNZA KUTOKA KWA BABA YAKO?
👉🏻Mwandishi Kiyosaki anasema kwamba Baba yake alikuwa mtu kubwa na mtu mwenye elimu ya hali ya juu.

👉🏻Anasema Baba yake alikuwa mwalimu wa shule ila kipindi Baba yake akiwa mwanafunzi hakutaka kusomea ualimu yeye alitaka kuwa daktari ila baada ya kuona watoto wengi wa wakulima wa miwa wanashindwa kusoma shule za private na wanasoma shule za serikali ambapo shule hizi zilipelekea wanafunzi wengi wa hali ya chini kuto fanikiwa katika masomo yao.

👉🏻Baba yake ndipo alipo amua kusomea ualimu ili kusaidia watoto masikini kufaulu na kusonga mbele kielimu na alikuwa na lengo la kubadili mfumo mzima wa elimu ili kusaidia jamii.

👉🏻Lakini pia Baba yake KIYOSAKI alimsisitiza mwanae ROBERT asome sana afaulu aende chuo halafu akimaliza masomo atapata kazi nzuri katika maisha yake.

👉🏻Lakini juhudi za Baba yake KIYOSAKI kubadilisha mfumo wa elimu na kusaidia watoto wanaosoma shule za  kimasikini/ Serikali hazikufanya vizuri kutokana na mabadiliko ya dunia kiujumla.

👉🏻Lakini badae Baba yake alipofikisha miaka 50 KIYOSAKI anasema alipo kuwa anarudi kutoka vietnam alimkuta Baba yake akiwa katika utata na mawazo na alikuwa anaona kama amesalitiwa na marafiki wenzake na mzee KIYOSAKI aliamua kustaafu mapema na kuanza kujaribu kufanya vibiashara fulani fulani kwa kutumia fedha alizo tunza na pensheni aliyo pewa,Baba yake wakati mwingine alikuwa anaketi tuu muda mwingi sebuleni ana angalia televisheni .

👉🏻Lakini KIYOSAKI alipo ona Baba yake katika hali ile akawa anakumbuka usemi wake kwamba soma uwe na degree,uwe na masters na kuendelea na upate kazi nzuri.

👉🏻KIYOSAKI anasema kikubwa alichojifunza ni kwamba shule hizi huwa hazimuandai mtu kukutana na changamoto au maisha halisi ya Dunia,Shule zina muandaa mtu kuwa mwajiliwa basi hamna kingine, ndipo akaamua kutofuata ushauri wa Baba yake mzazi na akaanza kufuata hatua za Baba wa rafiki yake yule Rich Dad.

👉🏻Baada ya Baba yake kufa ndipo akachapisha kitabu cha RICH DAD POOR DAD bila shaka watu walishangaa na kuona kama hana heshima kwa Baba yake mzazi,lakini anasema kwamba kupitia Baba yake ndipo aliamua kuandika ukweli na uhalisia wa maisha.

👉🏻DONALD anasema Baba yake yeye alikuwa yuko vizuri na alikuwa Role model wake kwa mambo yote anasema alipokuwa anafanya jambo fulani alipo kuwa  anataka kukata tamaa Baba yake alikuwa ana mtia moyo kweli na kumhamasisha na anasema Baba yake alikuwa tofauti na Baba wa ROBERT.

👉🏻Baba yake DONALD hakuwa mtu wa malalamiko,alikuwa mpiga kazi na anajifunza kupitia kazi zake na majukumu yake pia na hata Anapo pitia  wakati mgumu alikuwa anajifunza pia.

👉🏻Donald anasema amejifunza mengi kwa Baba yake kwa sababu alikuwa ndio kiongozi wake katika maisha yote aliyopitia ya utoto wake kwa hiyo alikuwa anamsikiliza na anachukua ushauri wake vizuri.

👉🏻 Wewe unajifunza nini kwa Baba yako?
Niandikie hapa chini
..........................................................................
Je Baba yako anafaa kuwa kiongozi wako kwenye masuala ya fedha au yupo kama Baba yake KIYOSAKI. Kama Baba yako hajakidhi mahitaji ya elimu yako ya fedha tafuta mentor au Baba mwenye kukidhi haja zako tengeneza urafiki naye atakufundisha na utajifunza mengi kwa huyo!

👉🏻Know everything you can about what you're doing!


              YOU MUST BECOME A RICH
              Ahsante,
      Usikose kesho sura ya kumi na tano ya kitabu.
            Phone.0742364499.
Email.mwanyikajackson428@gmail.com.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]