Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]

Tokeo la picha la WHY WE WANT YOU TO BE RICH by DONALD J. TRUMP & ROBERT T.KIYOSAKI.
        TWO MEN ~ ONE MESSAGE

        SEHEMU YA PILI

 SURA YA KUMI
WASHINDI WANACHUKUA UDHIBITI
👉🏻Mwandishi KIYOSAKI anasema kuelewa ni jinsi gani unaweza kufanya makubwa kwa kutumia nguvu ndogo kama ile sheria ya 80/20 ya kufanya vitu ambayo ameelezea Bwana BRIAN TRACY katika vitabu vyake maana yake utaanza kutumia mfumo huo katika kila mambo unayoyafanya katika maisha yako.

👉🏻Ukweli ni kwamba unapokuwa na mtu wa karibu kama msaada kwako unakuwa umefanya upanuzi wa fursa hapa ndipo tunaita rasilimali watu,ina maana unaweza kutumia rasilimali za watu wengi kukusaidia wewe katika mambo ya maisha yako!

👉🏻Ujumbe muhimu ni kwamba masikini wanatumia upanuzi mdogo na nguvu nyingi ukilinganisha na matajiri ambao huwa wanatumia nguvu zao binafsi kidogo kupata makubwa kwa kutumia nguvu za watu wengine.
Ukweli ni kwamba watu wa sehemu B na I huwa wanatumia upanuzi mkubwa hasa kwa kutumia muda na fedha za watu wengine!

👉🏻Upanuzi huwa upo katika aina mbalimbali mfano mawazo yako au fikra zako zaweza kuwa ndio upanuzi wenyewe, watu ambao huonekana washindi huwa wako makini na mawazo au fikra zao na mara nyingi watu wa namna hii wao huwa hawafikirii kushindwa kwa sababu fulani fulani ila wao hufikiria wata wezaje kupata wanacho kihitaji katika muda fulani wa maisha yao.

👉🏻Katika nguvu ya udhibiti kwa watu wawekezaji halisi wao baada ya kupata upanuzi mkubwa katika maisha yao huwa wanahitaji udhibiti ambao ni wa muhimu sana katika kuendesha biashara zao!
Na watu wengi wanafikiri uwekezaji ni hatari hii ni kwa sababu huwa hawana udhibiti je na wewe unaona uwekezaji ni hatari?

ROBERT aliwahi kutolea mfano wa dereva anapokuwa akiendesha gari huwa ana hitaji udhibiti ili kuepukana na ajali katika udhibiti wake anahitaji mambo sita ambayo ni;

📌Steringi

📌Breki

📌Crachi

📌Sehemu ya gia

📌Leseni

📌Bima

👉🏻Waandishi wanasema wanapenda biashara ya kupangisha majumba kwa sababu hii biashara ina udhibiti ukilinganisha na biashara ya kuuza na kununua hisa na wanasema kwamba kama wewe unataka kuwa mwekezaji wa majumba au mjasiliamali una hitaji udhibiti wa aina sita ambazo ni;

📌Kipato chako

📌Gharama

📌Mali

📌Matumizi

📌Usimamizi

📌Bima

👉🏻Wanapozungumzia elimu ya fedha wanazungumzia elimu ya kujua kivipi utaweza kudhibiti haya mambo sita!Pia unaweza kujifunza jinsi ya kudhibiti uwekezaji wako kwa kupitia hiyo elimu utakayo pata na kama una udhibiti maana yake faida yako itaongezeka na hatari za biashara yako zitashuka!

👉🏻Hebu tuone ni sehemu gani watu huwa hawana udhibiti,
Watu wengi huwa wanajisikia hawana nguvu kwa sababu huwa hawa wezi kudhibiti kazi au vibarua vyao,Mwandishi anasema kwamba amekutana na watu walio wameachishwa kazi na watu hao siyo kwa sababu ni wabovu kazini ila ni kwa sababu kampuni yao imeuzwa na wameachishwa kazi,hata kwenye hisa na mifuko ya pamoja watu huwa hawawezi kufanya udhibiti wa mambo hayo.

👉🏻Ukweli ni kwamba kuna sababu tatu ambazo watu huwa wanafikiri kwamba uwekezaji ni hatari;

💥Hawana elimu ya kutosha ya fedha.

💥Wanawekeza sehemu ambazo hawana udhibiti nazo.

💥Wanachukia ushauri kutoka kwa wafanyabiashara wakawaida ambao hawajui udhibiti wa uwekezaji.

👉🏻Lakini bwana DONALD anaendelea kisisitiza kwamba ili uweze kuwa na udhibiti basi unahitaji elimu ya kutosha,unapojua kwamba sehemu fulani unatakiwa uwepo kwa muda mwafaka maana yake unaweza kujidhibiti mwenyewe katika suala la Muda.

👉🏻Ukweli ni kwamba maisha yetu hapa duniani yana hatari nyingine sana,ila tunasonga mbele kwa sababu tufanya chaguzi sahihi na kwa udhibiti mkubwa hususani katika swala kukata tamaa.

👉🏻Mambo yanayo fanana na udhibiti ni kama yafuatayo;Amri,uongozi,mamlaka,utawala na maamuzi,unaweza ukawa huwezi kudhiti vitu vingi sana ila ni vema ukajidhibiti!

👉🏻Hebu jichunguze maisha yako leo je unaweza kuchunguza unatumiaje siku yako na je unaweza kuelezea kwamba unatumiaje siku yako.Je pia unatumiaje fedha zako na katika uwekezaji wako!

 *Niandikie hapa chini au inbox ili nikusaidie pia kuhusiana na maswali haya hapa chini!

Je ni kipi unaweza kukidhibiti katika maisha yako?.........................................................
..................................................................
..................................................................


Je ni yapi unashindwa kuya dhibiti katika maisha yako?
..................................................................
..................................................................
..................................................................

👉🏻Brainpower is the ultimate leverage

      
            YOU MUST BECOME A RICH
             Ahsante,
      Usikose kesho sura ya kumi na moja ya kitabu.
      Phone.0742364499.
  Email.mwanyikajackson428@gmail.com.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]