Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]


            TWO MEN ~ ONE MESSAGE
Image result for WHY WE WANT YOU TO BE RICH by DONALD J. TRUMP & ROBERT T. KIYOSAKI
             SEHEMU YA TANO

  SURA YA ISHIRINI NA NANE

KWA NINI UNASHAURIWA AU UNATAKIWA KUWA NA BIASHARA YAKO BINAFSI?

👉Mwandishi wetu KIYOSAKI ameendelea kusema tofauti za Baba yake mzazi na Baba wa rafiki yake kwamba Baba yake mzazi alikuwa amefunzwa kuwa mwajiliwa basi ambapo ilikuwa ni tofauti na yule Baba wa rafiki yake ambaye alikuwa anapenda kuwa mjasiliamali.

👉Mwandishi wetu bwana KIYOSAKI anapenda sana ujasiliamali pamoja na kwamba ukiwa mjasiliamali unapitia changamoto nyingi lakini kupitia changamoto hizo ndipo unapojifunza mambo muhimu na uzoefu katika biashara yako na maisha yako kiujumla.

👉Lakini Mwandishi anasema mojawapo ya mambo ambayo yanawafanya watu wajione kama hawana ulinzi katika maisha yao hapa duniani ni kwa sababu shule hazifundishi udhibiti wa maisha yao,mfano mdogo tu kama wewe ni mwajiliwa maana yake huna udhibiti au kama unao basi ni kidogo tu kwa kile unachopata,utangazwaji wako,kuhitaji kuongezewa kipato au kuomba kwenda kujiendeleza katika masomo yako.

👉Ukweli ni kwamba watu wengi wanashindwa kuweka au kuwa na maono ya maisha yao kwa sababu hawana udhibiti na kazi zao,uwekezaji wao na kodi zao.
 Ni muhimu kujitengenezea udhibiti wa maisha yako

👉Je tutapata wapi elimu ya ujasiliamali na ujuzi?
Ukweli ni kwamba shule zetu hazifundishi zaidi kuhusu masuala ya ujasiliamali lakini waandishi wanasema kwamba tafuta shule ya fedha soma na tafuta kiongozi maalum ambayo atakufundisha na kukusimamia kufanya hiyo biashara yako kwa uzuri kabisa au unaweza kujiunga na NETWORK MARKETING.

👉Bwana KIYOSAKI anamaliza kwa kusema kuna aina mbili za watu duniani yani kuna watu ambao wanafuata ulinzi na wanaotaka uhuru na hawa watu wanao utofauti mkubwa sana,yani watu wanao hitaji ulinzi mkubwa ni sawa na wafungwa katika magereza.

👉Bwana TRUMP anasema kwamba yeye binafsi hawezi kumwambia mtu aanze kipi kwa sababu si kila mtu ni mjasiliamali japokuwa anaweza kuwa mfanyabiashara mkubwa tu.


👉Pia Bwana TRUMP anaendelea kusema kwamba mtu akija kwake moja kwa moja anaomba ushauri kwamba anataka kuwa mjasiliamali basi huwa hapendelei sana kumshauri kwa sababu ujasiliamali huwa kuna hatari kubwa zipo ambapo mtu kama hajajipanga inaweza kule matatizo.

👉Anasema huwa anaweza mshauri mtu kufanya biashara fulani kama anaipenda hiyo biashara katika maisha yake kwa sababu hii huwa ni kama garanti ya hiyo biashara kwa huyo mhusika,anasema aliwahi kumshauri mwanamke mmoja anaitwa KIM MOGULL katika biashara ya majengo na huyo mama alifanikiwa mapema na alianza utekelezaji baada ya masaa 24 kutoka alipo pata ushauri kutoka kwa bwana TRUMP,Alimshauri Bwana mmoja katika mchezo wa Golf ambapo pia Jamaa alifanikiwa kuwa mshindi mkubwa tu!

👉Katika mifano miwili hiyo hapo juu👆🏻👆🏻Ukweli ni kwamba hao watu walifanikiwa kwa sababu hizi mbili,

📍Kwanza,Unatakiwa kuwa vizuri kwenye mambo unayotaka kufanya katika maisha yako.

📍Pili,Unatakiwa kuwa unajihamasisha mwenyewe kwenye mambo ambayo umekusudia kufanya katika maisha yako.

👉Unapokuwa na biashara yako ni sawa na mti unao kuwa au kama kiumbe ambacho kinapitia majira mbalimbali ya mwaka kiangazi ,masika,kipupwe na nk na unaendelea kuongezeka kwa hiyo ni vema kuwa na udhibiti hususani katika biashara yako maana biashara ndio inayosimama badala yako ina maana kama biashara ina simama vema basi ina maana na wewe uko vizuri.

👉Pia ukiwa na udhibiti na biashara yako basi utakuwa huna sababu ya kuchukia watu wengine kwa sababu wajibu wote utakuwa juu yako wewe na ni jukumu lako wewe binafsi.

👉Ukweli ni kwamba neno UHURU ni neno zuri sana ila huwa lina gharama sana,Wafanyabiashara wakubwa wengi hawa ndio huwa wanafanya kazi zaidi kuliko waajiliwa ,lakini Bwana TRUMP anasema hata kama maboss hawa wanapiga kazi muda mrefu hajawahi kusikia wanasema wanataka kuajiliwa .

👉Je wewe unataka kumiliki biashara yako?
________________

👉Neno uhuru kwako lina maana ipi?
________________


.

                      YOU MUST BECOME A RICH
                      Ahsante,
     Usikose kesho sura ya ishirini na tisa ya kitabu.
                     Phone.0742364499.
      Email.mwanyikajackson428@gmail.com.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]