Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]

*Natumaini wote ni wazima na tunashukuru MUNGU kwa uzima na afya,niombe radhi kwa wote kwa kuchelewesha somo la leo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu,karibu tuendelee na somo la leo*
.Tokeo la picha la WHY WE WANT YOU TO BE RICH by DONALD J. TRUMP & ROBERT T.KIYOSAKI.

           *TWO MEN ~ ONE MESSAGE.*

                  SEHEMU YA TATU

 *SURA YA KUMI NA TISA*
JE ULIJIFUNZA AU UNAJIFUNZA NINI KWENYE BIASHARA UNAYOFANYA AU ULIYOWAHI KUFANYA?
👉🏻Mwandishi wetu ROBERT anasema huwezi kujifunza kuendesha Baiskeli kwa kusoma kitabu, vivyo hivyo hata kwenye Biashara ndivyo ilivyo ina maana huwezi kufanya biashara kwa kusoma vitabu vya masuala ya kibiashara.

👉🏻Vitabu na madarasa ni kwa ajili ya kuongeza maarifa mapya lakini biashara ni kama kuendesha baskeli unahitaji michakato na hatua zaidi za kufanya kabisa biashara yako.

👉🏻Kuna usemi mmoja unasema kwamba jinsi unavyokuwa mkubwa na kujifunza zaidi ndivyo inavyokuwa ngumu kuanguka katika biashara au jambo fulani unalofanya maana yake ukijua kuendesha baiskeli vizuri ina kuwa ngumu sana kuanguka kwa sababu utakuwa na ujuzi mkubwa katika kuendesha hiyo baiskeli.

👉🏻Mwandishi anasema siku zote biashara ambayo inakuwa haraka hata kufa huwa inakufa mapema,anasema wao kuna kipindi fulani walifanya biashara na wenzake ndipo walipo ona mafanikio yao kuwa makubwa wakanunua magari ya kifahari wote watatu yani yeye KIYOSAKI na wenzake wawili,na pia walikuwa wamepata wanawake wakuwa tumia.

👉🏻Kwa hiyo ndani ya miaka mitatu walikuwa masikini badae wakawa matajiri mwisho wakawa masikini zaidi,anasema walikuwa wamefanikiwa ila baada ya muda wakawa katika madeni makubwa kutokana na kupoteza fedha zao.

👉🏻Mwandishi anasisitiza tusome kitabu chake kinaitwa RICH DAD'S BEFORE YOU QUIT YOUR JOB, anasema kuna habari nyingi kuhusu ujasiliamali na wajasiliamali katika kitabu hiki, anasema kwamba inatakiwa kipato chako kinavyoongezeka inatakiwa na elimu ya fedha iwe inaongezeka.

👉🏻Lakini kibaya zaidi ni kwamba jinsi kipato cha watu kinavyo ongezeka ndivyo watu wanapoongeza matumizi na utumiaji mbovu wa fedha,pia mwandisha anasema haamini kwamba elimu ya darasani ina umuhimu mkubwa,anasema yeye alikuwa na furaha alipokuwa anapata C katika masomo yake.

👉🏻Mwandishi anasema ukitaka kujifunza na kufanya biashara kubwa vema ni vizuri kujenga tabia ya kujifunza kila siku kama hujawahi jifunza kipindi cha nyuma na hii ni muhimu tofauti na ile elimu ya darasani ambapo ukimaliza shule ndio mwisho wa kujifunza lakini katika biashara ni somo endelevu.

👉🏻Mwandishi wetu DONALD anasema pia yeye amejifunza mengi ila anasema yeye alifanikiwa katika biashara na ilimchukua miaka 30.

👉🏻Donald anasema kwamba ni muhimu kuwa na maono katika maisha yako, lakini maono pekee haya toshi maana yake ukiwa na maono utahitaji kuongeza vitu vingine kama mtazamo chanya,kufanyia kazi maono hayo mpaka iwe kweli.

👉🏻Je wewe umejifunza nini kwenye biashara ambazo umewahi kufanya, ulijifunza nini kwa rafiki,jirani au ndugu yako aliyefanya biashara na akashindwa kuendelea na biashara hiyo??
_______________________________________________

👉🏻Je umejifunza nini baada ya kufanikiwa katika biashara yako au mafanikio ya biashara ya mtu mwingine????
________________________________________________


                      YOU MUST BECOME A RICH
                      Ahsante,
     Usikose kesho sura ya ishirini ya kitabu.
                     Phone.0742364499.
      Email.mwanyikajackson428@gmail.com.


No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]