Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]

Tokeo la picha la WHY WE WANT YOU TO BE RICH by DONALD J. TRUMP & ROBERT T.KIYOSAKI.
WHY WE WANT YOU TO BE RICH by DONALD J. TRUMP & ROBERT T.KIYOSAKI.

             TWO MEN ~ ONE MESSAGE

                    SEHEMU YA TATU

                SURA YA KUMI NA TANO

JE UNAJIFUNZA AU UMEJIFUNZA NINI KUTOKA KWA MAMA YAKO MZAZI?
👉🏻Mwandishi wetu KIYOSAKI anasema kwa sababu Mama yake alikuwa anampenda kuliko mtu mwingine duniani hivyo alijifunza upendo na utu kutoka kwa Mama yake mzazi.

👉🏻Mama yake KIYOSAKI alifariki Dunia akiwa na umri wa miaka 48 na alikufa mapema kutokata na matatizo ya magonjwa ya Moyo na pia mama yake alikuwa anafanyakazi ya uuguzi hospitali kabla umauti haja mkuta.

👉🏻Kutokana na ucheshi aliojifunza kwa Mama yake alipokuwa uwanja wa vita kule Vietnam siku moja alikuwa katika helicopter ndipo alipokutana na watoto wadogo kati ya miaka 9-12 ambao walikuwa wakicheza jirani na helicopter aliokuwa akiendesha mbali kidogo na kijiji fulani huko Vietnam,ndipo alihisi kwamba wale watoto inawezekana wametumwa na maadui akajaribu kutaka kumuua mmoja wa wale watoto lakini badae akasikia sauti ya Mama yake ikimwambia sikukuzaa kwa ajili ya kutoa uhai wa watoto wa akina mama wengine ndipo akaacha kufanya vile na kuchukua mpira na kuchezanao wale watoto kama watu wakawaida.

👉🏻KIYOSAKI anasema alishangaa kusikia sauti ya Mama yake hii ni kwa sababu Mama yake alikuwa ana upendo na watu na hata kwa watoto wake kwa hiyo alijifunza mazuri kwa Mama yake ambayo yali msaidia katika maisha yake.

👉🏻Mwaka 1984 KIYOSAKI akapata mchumba wake ambaye alijulikana kama Kim anasema pia mwanamke huyu ana tabia ambayo inataka kufanana na Mama yake kwa hiyo pia ina msaidia yeye kufanikiwa katika maisha yao wote kama familia moja.

👉🏻Mwandishi DONALD pia anasema amejifunza mengi mno kwa Mama yake ila makubwa zaidi anasema Mama yake alimwambia maneno haya Mwamini MUNGU na wewe mwenyewe uwe mkweli katika maisha yako .

👉🏻Mama yake TRUMP ambaye aliitwa Mary Trump alimwambia mwanae ajiamini na pia amwamini MUNGU katika maisha yake ya mafanikio.

👉🏻Wewe je unajifunza nini kwa Mama yako mzazi?
Niandikie hapa chini!.
....................................................................
Kama hujajifunza mambo mazuri kwa Mama yako inawezekana kwa sababu tofauti tofauti ya wezekana Mama yako alikufa ungali mdogo au walitengana na Baba yako akaolewa na mwanaume mwingine na nk,tafuta Mama ambaye unaona utajifunza mambo ya msingi katika maisha yako!!!

 NB;Kumbuka mama yako ni mama hata kama ni kichaa au hakusoma au masikini au kwa namna yoyote ile mheshimu kama mama maana hakuna kama mama Duniani.

👉🏻Trust in God and be true to yourself!

                 
                YOU MUST BECOME A RICH
                Ahsante,
    Usikose kesho sura ya kumi na sita ya kitabu.
                 Phone.0742364499.
  Email.mwanyikajackson428@gmail.com.

Usikose kuacha maoni yako chini ya Blog:

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]