Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]


            TWO MEN ~ ONE MESSAGE
Tokeo la picha la WHY WE WANT YOU TO BE RICH by DONALD J. TRUMP & ROBERT T.KIYOSAKI.
             SEHEMU YA NNE

                INTRODUCTION

KAMA UNGEKUWA KWENYE KIATU CHA MOJA WAPO YA WAANDISHI WETU UNGEFANYAJE?
👉🏻Mwandishi wetu KIYOSAKI katika utangulizi wa sehemu ya nne anasema kwamba hatari kubwa anayoiona kwa watu ni pale mtu anapokuwa na fedha hajui afanyie nini! Na mtu huyo anauliza kwa watu mfano Nina 10000$ nifanye biashara gani??.

👉🏻Anasema mtu akiuliza swali kama hili atawavutia watu wengi sana ambao wanajua jinsi gani wata tumia fedha zako au fedha za mtu asiye jua jinsi ya kutumia fedha zake!

👉🏻Anasema watu wengi wanatoa njia kubwa mbalimbali za jinsi gani ya kuanza biashara fulani kutokana na hela ya huyo mtu na Mwandishi anasema watu wanao taka kushauriwa jinsi gani wata tumia fedha zao katika biashara ndio wale wanaochukua ushauri ya kwamba watunze fedha,watoke kwenye madeni,wawekeze kwa muda mrefu na wawekeze sehemu tofauti tofauti kutoka kwa washauri wa fedha.

👉🏻Kama unataka kupata ushauri kutoka kwa watu kuhusu masuala ya fedha basi utapata ushauri kwamba ishi chini ya viwango vyako na wata kwambia vitu vizuri ili tu  vitakufanya usianguke katika biashara hiyo unayoshauriwa kufanya.

👉🏻Na watu wenye ushauri wa namna hiyo wao huwekeza kupata na siyo kupoteza,hawapendi kukosea,hawependi kujifunza kutokana na makosa,na wewe kama unaogopa kufanya makosa basi tafuta ushauri wa namna hiyo.

👉🏻DONALD na ROBERT wao wanaamini katika elimu ya fedha na kujipanga zaidi na siyo kupata majibu au ushauri sahihi kutoka kwa watu, na wanasema wao wanaishi katika viwango vyao na hupanua wigo wa viwango vyao na siyo kuishi chini ya viwango vyao.

👉🏻Katika sehemu hii ya nne ya kitabu waandishi wetu wanatupa motisha kwa kushauri sisi kusonga mbele kwenye masuala ya fedha kwa kutupa elimu ya fedha na jinsi ya kujiandaa katika masuala ya biashara zetu.


                      YOU MUST BECOME A RICH
                      Ahsante,
     Usikose kesho sura ya ishirini na moja ya kitabu.
                     Phone.0742364499.
      Email.mwanyikajackson428@gmail.com.



No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]