*TWO MEN ~ ONE MESSAGE*
.

SEHEMU YA NNE
*SURA YA ISHIRINI NA TATU*
WEWE UNA MIAKA KATI YA 50 HADI 70 NA HUNA FEDHA NYINGI JE UNA NATAKIWA KUFANYA NINI?
👉🏻Mwandishi anasema watu walio zaliwa kati ya 1946 na 1964,watu hawa ni wazee wetu na wamezaliwa kipindi ambacho nchi ya Marekani ikiwa imetawala Dunia kiuchumi na kijeshi,lakini leo hii wao wenyewe ni mashahidi kwamba Marekani inashuka kiuchumi na kama siyo uchumi basi inashuka kijeshi.
👉🏻Kizazi hiki ni kizazi cha mwisho katika zama za viwanda na ni cha kwanza katika zama za tarifa au habari,hiki kizazi ndio hiki kinaitwa kizazi cha mpito na mpito huu ndio umegawanya kizazi hiki kati ya wenye fedha na wasio na fedha.
👉🏻Mwandishi anasema watu wenye umri huu ambao wamebadilika na kuendana na zama hizi za habari wana nafasi kubwa wanapo staafu kuwa na maisha mazuri kwa sababu wataendana na sheria za zama hizi. Mfano wale waliochagua kufanya kazi kwenye baadhi ya viwanda leo watakuwa kwenye utata wa maisha yao lakini wale ambao walichagua kufanya kazi kwenye kampuni mfano kampuni ya microsoft wanauafadhali .
👉🏻Ukijaribu kuchunguza kizazi hiki wanapata tabu sana hata kupata pesheni yao kwa sababu zama zimebadilika kutoka mwaka 1974, na wengine wanapo bahatika kupata pesheni basi huwa wanashindwa kuwekeza wanawapa watu ambao wanajifanya ni watu wa masuala ya fedha matokeo yake wanapoteza fedha zote hii ni kwa sababu tu wao hawana elimu ya fedha ya kutosha.
*AFYA,UTAJIRI NA FURAHA*
👉🏻Mwandishi anasema kwamba Baba yake alikuwa mtu mwenye mafanikio kama wanavyojiona waajiliwa wengine kwamba Baba yake alikuwa na elimu kubwa,anatoa huduma nzuri na anaheshimika na marafiki zake wa rika moja,lakini KIYOSAKI anasema hakuwa na Afya,
Tajiri wala furaha huyo Baba yake.
👉🏻Anasema Baba yake alikufa kwa kansa ya mapafu hii ni kwa sababu alikuwa anavuta sigara,pia hakuwa tajiri ingawa alikuwa anatengeneza fedha nyingi za kutosha ila fedha hizo alikuwa anatumia zote katika maisha ya kila siku. Na alikuwa ana tabia ya kutunza fedha na siyo kuwekeza fedha na yeye alikuwa anahesabu kwamba ana bima na pia ana peshion akisha staafu kazi.
👉🏻Hakuwa na furaha na jinsi alivyokuwa anazidi kufanikiwa ndivyo muda mwingi alikuwa anahitajika kazini hakuwa na muda na familia yake na nyumbani alikuwa anapatikana kwa bahati sana.
👉🏻Ni rahisi kupima AFYA na UTAJIRI wa mtu ila ni ngumu kupima FURAHA ya mtu,unapokwenda kwa Daktari akichukua Damu yako na Kupima Pressure yako au akakuweka na kuchukua vipimo kwa kutumia MRI hapo ndipo unaweza kujua AFYA yako ikoje. Hii ni sawa na kwenye masuala ya UTAJIRI, kama mtu wa benki akitaka kujua kuhusu masuala ya fedha au benki wakitaka kukukopesha basi huwa wanauliza kuhusu Maelezo ya kifedha.
👉🏻Pia masuala ya UTAJIRI na AFYA hupimwa na muda mfano ukienda kwa Daktari akakwambia una miezi sita ya kuishi maana yake ni kwamba AFYA yako ni mbaya,pia kama wastani wa kuishi ni miaka 75 na wewe una miaka 60 ina maana uko nje ya muda.
👉🏻Katika gazeti la Forbes Tajiri maana yake ni mtu mwenye dolla millioni moja na zaidi kama kipato cha mwaka kumbe tajiri anapimwa kwa fedha alizo kuwa nazo lakini,utajiri au mali unapimwa kwa muda.
👉🏻Kuna uhusiano mkubwa kati ya AFYA, MALI NA FURAHA,upokuwa na mali na afya hii ina kufanya uishi muda mrefu katika maisha yako ukilinganisha na watu masikini.
👉🏻Tatizo kubwa katika jamii ni kwamba watu wanajitoa sadaka kwa kuto linda AFYA za miili yao kwa ajili ya kupata mali na fedha,waajiliwa walio wengi wanafanya kazi kwa nguvu bila kulinda AFYA zao kama alivyokuwa anafanya Baba yake ROBERT.
👉🏻Kama wewe umezaliwa au ni mtu wa kizazi cha 1946-1964 na huna fedha za kutosha basi fanya mambo haya matatu yata kusaidia.
📌Kwanza,Kama uko kazini na bado huja anza kufanya kitu fulani unachotaka au unachofurahia anza mara moja hata kwa kutumia muda wa ziada ili ukistaafu uwe tayari una ujuzi na hicho kitu.
📌Pili,anza kuwekeza kwenye vitu unavyopenda katika maisha yako na usiwekeze kwenye vitu ambavyo huvijui.
📌Ajili kocha au uwe na mentor atakaye kuongoza katika maisha yako na vile unavyovipenda.
👉🏻UPENDO ni ufunguo wa maisha yenye AFYA, MALI NA FURAHA,ni rahisi kuwa na afya kama unafurahia maisha yako na ni rahisi kuwa na MALI kama una furaha, kibaya zaidi wengi wanaweka uoga badala ya kupenda mambo wanayoyafanya.
👉🏻Upendo huwa hauji kirahisi,Upendo huwa na gharama na wakati mwingine kupenda huwa kuna maumivu makubwa,watu wengi wanapenda kazi,wapenzi au hata ndugu zao lakini kuna wakati mambo hayo hayo huwapa maumivu makubwa,kumbe upendo si rahisi kuja lakini una maana kubwa kwenye maisha ya watu duniani.
👉🏻DONALD anasema kama umri umekuacha panga malengo yako upya na ufanye vitu unavyovipenda na kama huna fedha za kutosha basi shukuru kwa uzima ulio nao na uhai wako kwa maana bado una nafasi ya kufanya mambo mengine makubwa katika maisha yako.
👉🏻Don't understimate yourself or your possibilities.
YOU MUST BECOME A RICH
Ahsante,
Usikose kesho sura ya ishirini na nne ya kitabu.
Phone.0742364499.
Email.mwanyikajackson428@gmail.com.
No comments:
Post a Comment