
Moja ya ukweli ambao lazima uukubali ni kuwa si kila mtu atakuwa na wewe Muda wote wa Maisha Yako.Kuna watu utakuwa nao karibu sana leo lakini utashangaa kesho mnapoteana,Kwa Nini?
.
1)Kinachowaunganisha hakipo tena(Common Interest).
.
Kuna ukaribu ambao unaunganishwa na vitu vya pamoja ambavyo kwa wakati huo wote mnavithamini:Inawezekana ni kusoma pamoja,kushabikia timu moja,Kuhudhuria Nyumba moja ya Ibada,kufanya kazi pamoja n.k.Unachotakiwa kujua ni kuwa mambo haya yanaweza kubadilika na kufanya Msiwe karibu tena.Ukigundua mabadiliko haya usilazimishe ukaribu,tambua wakati umefika muachane kwa amani bila ugomvi.
.
2)Hisia kuchoka(Emotional Fedup)
.
Kuna wakati mtu anaweza kuvumilia Kitu hadi ikafika kiwango ambacho hawezi tena kuvumilia na Hisia zimechoka.Kwa wakati huu wengi huona Njia rahisi ya kuwasaidia ni kuweka umbali na mtu husika.Hii inamaanisha hata kama zamani Hisia zilikuwa juu sana lakini kutokana na mambo yaliyotokea ama maneno fulani,zile Hisia zinapotea.Ukijua tatizo hili na kama bado huyu mtu unamuhitaji kuna Njia unaweza kutumia kurudisha ukaribu.(Nimeeleza hili kwenye kitabu cha NGUVU YA MWANAMKE sura ya Tano)
.
3)Kujiona wa Muhimu kuliko kila mtu(Personal Ego)
.
Kuna watu unawaacha/wanakuacha kwa sababu wanajiona wako bora kuliko kila mtu.Watu hawa tunasema “they are so full of themselves”.Huwa wanajivuna kila wakati,hawapendi kukosolewa na hawasikilizi wengine.Wao hukuona wewe UNAJIPENDEKEZA kila siku.Wanataka uwasifie na utengeneze Muda kwa ajili yao ila wao huwa HAWANA MUDA na wewe.
.
Je,Umeshawahi kuondoka kwenye maisha ya mtu kwa sababu yoyote kati ya hizi???KUMBUKA:Unaweza kuachana na mtu kwa AMANI sio LAZIMA KUWE NA UGOMVI ama KURUSHIANA MANENO.">
No comments:
Post a Comment