*TWO MEN ~ ONE MESSAGE*
.

SEHEMU YA NNE
*SURA YA ISHIRINI NA MOJA*
BADO NIPO SHULE .......JE NATAKIWA KUFANYA NINI?.
👉🏻Mwandishi anasema kama wewe bado ni kijana upo shule anasema jaribu kuangalia kitu gani unakipenda katika maisha yako,halafu jifunze hicho kitu vizuri.
👉🏻Anasema utakuta wazazi wanawapeleka watoto kwenye shule kubwa au vyuo maarufu anasema yeye kwamba kama angekuwa mtoto wao asingependa kabisa pia anasema yeye alikuwa masikini na anatoka katika familia masikini lakini alikuwa anataka kuwa tajiri katika maisha yake lakini wazazi na familia yao walikuwa wanafikiri kuwa tajiri ni dhambi na siyo kitu chema.
👉Tunashauriwa kama umezaliwa kwenye familia ambayo ina waza vibaya kuwa tajiri au kuhusu utajiri tafuta rafiki kwenye mtandao au mtu mwingine yoyote ambaye utakuwa unashirikiana naye kwenye mambo ya biashara na heshima nyumbani acha iendelee bila kuharibu uhusiano na wazazi wako kwa sababu familia yako ni muhimu sana pia.
👉🏻Kama familia yako inapenda utajiri basi mnaweza kuwa pamoja kwenye mambo ya kibiashara na mambo yote yanayo husiana na utajiri kwa pamoja.
👉🏻Cha msingi ni kwamba fedha pekee haiwezi kuwa na mabaya,na tunajua kabisa watu wengine wanafanya mambo mabaya kwa ajili ya fedha, watu wengi wanafikiri kama watakuwa wanapenda fedha basi watakuwa wachoyo ambapo baadhi ya watu wanafanya ambao ni matajiri
👉🏻Kama umeamua kuwa tajiri au Mtu mwenye fedha za kutosha basi unaweza kuchagua kuishi vyema kwa kujitolea bila kuwa mchoyo eti kwa sababu una fedha.
*CHANGAMOTO MBILI KUU ZA SHULE*
📌Shule ina muandaa mtu kwa ajili ya kufanya vibarua au kazi,watu wengi leo hii wanahangaika kupata fedha hii ni kwa sababu wakiwa shule walifundishwa kufanya kazi ili wapate fedha.Ni wachache ambao wamefundishwa kwamba fedha inatakiwa iwafanyie kazi wao.
📌Pili shuleni wanafunzi wanapigwa pindi wanapofeli kwenye mitihani au kama wakikosea,anasema mtu anapojifunza kuendesha baiskeli akianguka halafu ukampiga ina maana mtu hawezi kuendelea kujifunza kwa sababu atakuwa anaogopa kupigwa,kwa hiyo njia kubwa ya kujifunza mambo ni kujifunza kupitia makosa unayofanya!
👉🏻Mwandishi anasisitiza pia kuwa na kiongozi wako maalum ambaye atakuwa mshauri wako katika maisha yako na siyo kuwa na Mwalimu, kwa sababu mwalimu huwa anafundisha masomo na kiongozi wako yeye anakuongoza kwenye mambo unayo yapenda Katika maisha yako.
👉🏻Mwandishi anasema ni muhimu kusoma shule na vyuo kwa sababu ambazo yeye ameona mfano.
📌Unapokuwa shule au chuoni ni sehemu ya kukua na kujifunza .
📌Unapo pata degree ni tiketi ya kufanya vitu fulani mtaani, mfano anasema yeye alipokuwa jeshi kama Ruban degree yake ilikuwa ni tiketi ya yeye kwenda kwenye vita vietnam lakini kulikuwa na marubani wengine wazuri kuliko yeye lakini walimchukua kwa sababu yeye alikuwa ana degree tayari.
📌Unapokuwa chuo unatambua mambo gani unapenda na yapi huyapendi katika maisha yako.
👉🏻Anasema wanafunzi wengi walipo muuliza swali ya kwamba wasome nini?
Anajibu kwa ni muhimu kusoma mambo makuu mawili yatakusaidia katika biashara na maisha yako.
📒Accounting
📒Business law
👉🏻Anasema ni muhimu kusoma hayo mawili kwa sababu yana msaidia mwanafunzi kujua na kuona biashara au kuwekeza sehemu fulani bila watu wakawaida kuona mapema na nakujua fursa mapema yani mwanafunzi anakuwa kama na miwani ya X ray ambapo anaona fursa wengine hawaoni kabisa.
👉🏻Faida nyingine mtu anakuwa na nidhamu kama professions nyingine mfano lugha ya kidaktari au ya uwalimu .
👉🏻Pia mtu akiwa na elimu hiyo anakuwa anajua kuhusu matumizi,mali na mzunguko wa fedha.
👉🏻Anasema kujua kuhusu mzunguko wa fedha ni muhimu kwa sababu ndio msingi wa udhibiti kwa mwekezaji na mjasiliamali,wawekezaji walio wengi wanaona kama kuwekeza ni hatari hii ni kwa sababu hawana udhibiti katika uwekezaji,kwa hiyo mzunguko wa fedha ni muhimu kwa mwekezaji mkubwa na mjasiliamali wa uhakika.
👉🏻Watu wengi leo wapo kwenye shida ya madeni na wanaumia kuhusu fedha ni kwa sababu hawajui kuhusu mzunguko wa fedha yani kiasi kinacho ingia kama kipato na kiasi kinachotoka kama matumizi,matokeo yake upande wa matumizi unakuwa mkubwa kuliko mapato na ndio maana wanaingia kwenye hasara.
👉🏻Alama moja wapo ya kujua kwamba mtu ana akili nyingi kuhusu masuala ya fedha ni kwa kuangalia kwamba upande wa mapato kuwa na mapato mengi yana ingia kuliko matumizi yanayotoka
👉🏻Pia anasema kwamba wafanyabiashara ya uwekezaji majumba na wajasiliamali wanapata fedha nyingi hii ni kwa sababu wanaujuzi ambao unawafanya wao waweze kuwekeza katika majumba na biashara.
👉🏻Mwandishi anasema kwamba kama utaweza kuwa na bajeti,kuwa na udhibiti wa mzunguko wa fedha ili fedha iwe inaingia kwako,utakuwa na nafasi nzuri ya kuwa tajiri katika maisha yako.
👉🏻DONALD anasema ni vizuri kuwa na mshauri au mentor wako ambaye atakuongoza kwenye maisha yako na vitu unavyotaka kufanya. Pia anasema ni muhimu kufanya zaidi ya matarajio yako unapotaka kufanya kitu fulani.
👉Mwandishi wetu DONALD anasema soma na uendelee kujifunza zaidi na zaidi kwa kadiri uwezavyo katika maisha yako kwa kile unachokipenda na haijalishi umefika nafasi gani ya elimu endelea kujifunza zaidi kila siku.
👉🏻Kama upo chuo usisubiri fursa zikufuate anza kidogo kidogo mpaka utafanikiwa kamwe usisubiri fursa zije ndio uchukue maamuzi.
👉🏻Pia anasema ni muhimu kuendeleza elimu yako ya fedha na kujitathimini kila wiki hii itakujengea uwezo wa kujua zaidi kuhusu masuala ya biashara.
👉🏻Mwandishi anasema tumia muda fulani kujitazama na kujigundua unapenda nini katika maisha yako pia ametuachia maswali mawili
📌Kwanza, utafanya kitu gani kama hutaki fedha(bila kuhitaji fedha)?
______________________________________________
📌Utafanya kitu gani kama unajua hutaanguka au kufeli(yani kukosea)?
________________________________________________
👉🏻Do not neglect your life skills,which should include a healthy dose of financial education.
YOU MUST BECOME A RICH
Ahsante,
Usikose kesho sura ya ishirini na mbili ya kitabu.
Phone.0742364499.
Email.mwanyikajackson428@gmail.com.
No comments:
Post a Comment