*TWO MEN ~ ONE MESSAGE*
.

SEHEMU YA TANO
*SURA YA ISHIRINI NA SITA*
KWA NINI UNATAKIWA KUWEKEZA KWENYE BIASHARA YA MAJUMBA??
👉🏻Mwandishi yeye anawekeza kwenye biashara ya majengo anasema jibu lake huwa liko katika neno moja tu ambalo ni *Udhibiti* ,anasema hakuna uwekezaji mwingine zaidi ambao unaweza ukawa na udhibiti mzuri wa fedha na kumpa fedha na ukamasidia kudhibiti hata maisha yake!
👉🏻Anasema kama alivyosema mwanzo watu wengi wana ogopa kuwekeza hii ni kwa sababu wanadhani kwamba uwekezaji ni hatari na unaweza kuwapa hasara,na matokeo yake wanawekeza kwenye mifuko ya pamoja na mambo yanayo husiana na hisa ambayo hayana udhibiti wa moja kwa moja.
Kumbuka;
*RISK = ~CONTROL~*
👉🏻Watu wana wasiwasi na ulinzi wa kazi zao hii ni kwa sababu hawana udhibiti na kazi zao.Pamoja na kwamba uwekezaji wa majumba unakupa udhiti wa uwekezaji wako
Pia una faida zifuatazo kama nyongeza ,
📌Mzunguko wa fedha,kila mwezi unalipwa fedha.
📌Unatumia nguvu kidogo kupata fedha nyingi,kwa sababu benki pia wanaweza kukukopesha kwa sababu unakuwa na dhamana.
📌Kama umekopa mkopo benki basi mpangaji ndio anayelipa deni lako.
📌Kodi kwa serikali ni ndogo sana
📌Unapokuwa na ubunifu katika majengo yako na biashara hii ni rahisi na pia inakupa ubunifu zaidi
📌Kutokana na kwamba biashara hii unapata mikopo benki kirahisi unaweza kuongeza majengo mengine mengi kwa kupitia jengo moja la kwanza
📌Unaweza kuwa na makadiliko ya kufanya biashara yako na kitu kikubwa unahitaji kuwa na uongozi na usimamizi safi kabisa.
📌Kodi yake inapunguzwa
📌Unapata faida sawa na biashara nyingine.
👉🏻Mwandishi anasema ameweka faida kuwa ya mwisho kwa sababu ukiangalia biashara nyingine watu wanaangalia faida kwanza,unapokuwa unafanya biashara kwa kuangalia faida ni sawa na kubashiri mechi au kutabiri biashara yako,kumbe basi faida inatakiwa kuwa mwisho kabisa wa mawazo yako.
👉🏻Pia anasema kwamba siri nyingine inayomfanya apende kuwekeza kwenye majengo ni kwamba pamoja na kwamba yeye ni mtu wa kizazi cha zamani,Anasema anapowekeza kwenye majengo hawezi kupitwa na Dunia kwa haraka kwa sababu uwingi wa watu unaongezeka na watu wanahitaji sehemu za kuishi kwa hiyo hata kama kunakuwa na mabadiliko ya sayansi na teknologia bado watu wanahitaji sehemu za kuishi.
👉🏻Ukweli ni kwamba pamoja na kwamba unakuwa na majengo yako kwa kupangisha kibiashara bado kwa sababu ardhi inamilikiwa na serikali kwa hiyo lazima unalipa kodi ya mali au hayo majengo yako.
👉🏻Nguvu ya kuwa na maono,kwenye biashara ya majengo na nyingine, kama mtu anakuwa na elimu na uelewa kuhusu fedha basi mtu huyo huwa anakuwa na maono ya kibiashara kuliko wengine au mwenzake. Na anasema wao wanawekeza katika majengo kwa sababu wanaona mzunguko wao wa fedha hii ni tofauti na uwekezaji wa bondi,hisa au mifuko ya pamoja.
👉🏻Unapowekeza kwa muda mrefu unakuwa huoni kinachoendelea katika uwekezaji wako
*mfano*
unapowekeza kwenye kampuni fulani kwenye mifuko ya pamoja kama ukiwekeza kwa miaka zaidi ya 40 inakuwa kama ifuatavyo;
*Kampuni ya *Wewe*
*mifuko ya pamoja* .* *mwekezaji*
Faida 80%. Faida 20%
Hasara au hatari 0%. Hatari 100%
Mtaji 0%. Mtaji 100%
👉🏻Ukiangalia hapo ndio maana una pata jibu kwamba kwa nini benki hawa wezi kumkopesha fedha mwekezaji wa mfuko wa pamoja.
👉🏻Mwandishi wetu DONALD anasema unapowekeza kwenye majengo ni mojawapo ya sehemu kubwa ambayo unaweza kuweka fedha zako kwa usalama,hata kama kuna kushuka na kupanda katika biashara hii bado ni tofauti na biashara nyingine.
👉🏻Pia Mwandishi wetu DONALD anasisitiza kujua unapenda nini katika maisha yako maana yeye alikuwa anapendelea kuwekeza katika biashara za majumba na kupangisha pia.
👉🏻je wewe unapenda nini katika maisha yako, unapenda kuwekeza katika sehemu ipi na unaifurahia????________________________________________________
👉🏻People with vision master the ability to see through to the heart of issues and investments.They value transparency.
YOU MUST BECOME A RICH
Ahsante,
Usikose kesho sura ya ishirini na saba ya kitabu.
Phone.0742364499.
Email.mwanyikajackson428@gmail.com.
No comments:
Post a Comment