Full width home advertisement

Travel the world

Post Page Advertisement [Top]



           *TWO MEN ~ ONE MESSAGE*
.Tokeo la picha la WHY WE WANT YOU TO BE RICH by DONALD J. TRUMP & ROBERT T.KIYOSAKI.
             SEHEMU YA NNE

 *SURA YA ISHIRINI NA NNE*

JE KAMA WEWE TAYARI NI TAJIRI?UNATAKIWA KUFANYA NINI?!
👉🏻Mwandishi wetu KIYOSAKI anasema kama umekuwa tajiri tayari jua umebarikiwa ila tukumbuke kwamba kuwa na fedha nyingi inaweza kuwa baraka au laana.

👉🏻Watu walio wengi duniani ambao wanafedha nyingi huwa zinawaletea matatizo, yani kama una fedha nyingi wakati mwingine huwa ni matatizo katika jamii,unapokuwa na fedha nyingi lazima utatakiwa ujue jinsi ya kuhifadhi na kuzilinda,pia unakuwa  kama mtu anayehitajika na watu wengi wanao hitaji fedha zako.

👉🏻Unapokuwa una angalia  CASHFLOW game board utaona kuna aina tatu za wawekezaji ambao ni;

📌Wawekezaji ambao wanapambana kupata utajiri na mali,hawa ndio wengi na wawekezaji ambao wao wanawekeza katika mifuko ya pamoja na hisa tofauti tofauti na hawana elimu ya fedha kabisa.

📌Wawekezaji wenye mikataba midogo na mikubwa,hawa wawekezaji wengi wao wana elimu ya fedha na wao angalau siyo kama hao wanao wekeza kwenye mifuko ya pamoja.

📌Wawekezaji ambao wanafanikiwa haraka au kwa wakati mwafaka,hawa ni Wawekezaji wenye elimu ya fedha na wana ujuzi wa biashara hawa wamegawanyika katika makundi mawili;

💥Kwanza,Matajiri au watu wenye fedha na pia wanaelimu ya fedha ambayo ina wasaidia wao kuwekeza na kufanikiwa haraka sana katika maisha yao.

💥Pili,Matajiri au watu wenye fedha lakini hawana elimu ya fedha ya kutosha na ujuzi pia hawana.

👉🏻Mwandishi anasema watu waliojitengenezea utajiri wao wenyewe bila kutegemea sehemu yoyote huwa hawaogopi kufirisika au kuanguka katika biashara zao.

👉🏻Unapo wekeza katika uwekezaji ambao unakusaidia wewe kufanikiwa mapema huhitaji ulinzi mkubwa wa fedha zako na unapata faida kubwa.

👉🏻Mfano wa uwekezaji huo ni kama ifuatavyo;

📒Unapoanza biashara kama mjasiliamali na ukapewa fedha kutoka kwa wawekezaji wakubwa.

📒Uwekezaji katika majumba na kuwa na ushirikiano na watu wengine wanao wekeza katika majengo.

📒Uwekezaji katika mafuta na gesi,hapa unajihakikishia kuwa na mzunguko wa fedha na pia kodi yake siyo kubwa,

👉🏻Kama wewe ni tajiri kazi yako kubwa katika fedha zako ni kuhakikisha unaziongeza haijalishi unafanya kitu gani na pia ni muhimu sana kuwa na mambo yafuatayo.

💥Mapenzi na hizo fedha zako

💥Kuwa na mipango kuhusu hizo fedha

💥Kuwa na mpango mbadala kama kuna kitu kinashindikana kwenye mpango ule wa kwanza.

💥Kama limetokea tatizo au kuanguka katika biashara lazima kuwe na mpango au makubaliano ya kuhakikisha biashara inakuwa na kurudi mahala pake.

👉🏻DONALD anasema kwamba hongera kama umekuwa tajiri tayari ila pia anakuasa wewe tajiri kwamba uwe makini na hizo fedha na jinsi ya kutumia pia.

👉🏻Kwa hiyo DONALD anasema ili uendelee kufanikiwa zaidi lazima ujenge tabia ya kujifunza mara kwa mara ili uwe na miradi mingi zaidi na zaidi,pia jua majukumu yako na kuwa na mtazamo chanya katika maisha yako na mafanikio yako.

👉🏻If you are not doing what you love,then start doing it,even if it is only part-time.



Hali ya maisha sasa hivi imekuwa ni tofauti, makampuni yanabana matumizi hivyo nasisi lazima tubane matumizi. Hizi ni mbinu unazoweza kuzitumia kubana matumizi

1. Ukifanya maamuzi ya kuishi tafuta mahala ambapo ni karibu na ofisini kwako

2. Ukiwa ndani ya nyumba zima taa katika vyumba ambavyo havitumiki

3. Kama una mahusiano mazuri na wafanyakazi na mnakaa karibu wekeni mpango wa kutumia gari moja ili mchangie mafuta

4. Epuka kula nje ya nyumba ukiweza pika mwenyewe nyumbani.

5. Chagua harusi za kuchangia usichangie kila harusi kisa umeletewa kadi.

6. Badala ya kulipia channel 150 kwenye king'amuzi lipia channels unazoangalia tu

7. Badala ya kulipia gym jiunge na jogging clubs na fanya mazoezi mwenyewe (programs zipo kwenye internet)

8. Ukitoka out na mtu mwambie kuwa kila mtu atajilipia bili yake

9. Ukienda kazini toka na baadhi ya vyakula ambavyo mjini ni gharama au havipatikani kama matunda

10. Mtu akikuomba hela ghafla pima uzito wa maombi vinginevyo mwambie haiko kwenye bajeti mpaka utakapopanga bajeti nyingine.

11. Ukinunua taa nyumbani nunua zinazotumia umeme kidogo

12. Usipende kutembea usiku lolote linaweza likatokea likakugharimu pesa

13. Usipende kuazima kitu cha mtu kikipata tatizo huna namna zaidi ya kulipa wakati ambao hauna hiyo bajeti

14. Nguo unazoweza kufua nyumbani usipeleke dry cleaner.

15. *Usisahau kuabudu na kumtolea Mungu Zaka na Sadaka*

                    YOU MUST BECOME A RICH
                      Ahsante,
     Usikose kesho sura ya ishirini na tano ya kitabu.
                     Phone.0742364499.
      Email.mwanyikajackson428@gmail.com.
*BADILI MFUMO WA MATUMIZI *


No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]